Pata taarifa kuu

Guinea: Rais wa zamani Alpha Condé aondoka Conakry na kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu

Kulingana na duru za kuaminika, ndege iliyombeba rais wa zamani wa Guinea, Gulfstream G-IV, imeondoka kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ahmed Sekou Touré Jumatatu hii Januari 17, mapema alasiri.

Aliye kuwa rais wa Guinea Alpha Conde.
Aliye kuwa rais wa Guinea Alpha Conde. REUTERS/Afolabi Sotunde/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Alpha Condé alipata ruhusa kutoka kwa Mamadi Doumbouya kuondoka nchini ili kupokea matibabu huko Abu Dhabi. Ameambatana na daktari wake, Dkt Kaba, na walinzi wawili.

Ndege yake, iliyoondoka Jumatatu Januari 17, 2022, inatarajiwa kuwasili Abu Dhabi. Mkuu huyo wa zamani wa nchi hapo awali alikuwa amepata idhini kutoka kwa mamlaka ya mpito kuondoka nchini kwa matibabu kwa muda wa mwezi mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.