Pata taarifa kuu

Guinea: Rais wa zamani Condé na mawaziri kadhaa wa zamani kufunguliwa mashitaka ya ufisadi

Utawala wa kijeshi nchini Guinea umeagiza leo Alhamisi kuanzishwa kwa kesi za kisheria dhidi ya rais wa zamani Alpha Condé ambaye utawala wake uliangushwa katika mapinduzi ya 2021, na zaidi ya maafisa wakuu 180 au mawaziri wa zamani, hasa kwa tuhuma za vitendo vya ufisadi, kulingana na barua ya umma kutoka Waziri wa Sheria kwa wanasheria wakuu.

Rais wa zamani wa Guinea Alpha Condé.
Rais wa zamani wa Guinea Alpha Condé. REUTERS/Afolabi Sotunde/File Photo
Matangazo ya kibiashara

“Mnaagizwa (...) kuanzisha kesi ya kisheria (...) kwa tuhuma za vitendo vya “rushwa, kujitajirisha kinyume cha sheria, utakatishaji fedha, makosa ya kughushi nyaraka na kutumia nyaraka za kughushi na ubadhirifu wa fedha za umma," barua hii imebaini. Majina ya watu 188, likiwemo lile la rais wa zamani Condé na Waziri Mkuu wake wa zamani Ibrahima Kassory Fofana, ambao akaunti zao za benki zimefungiwa, yameambatanishwa na barua hiyo.

"Serikali ya Guinea, katika sera yake ya kuadilisha maisha ya umma, imejiwekea lengo la kupambana na makosa ya kiuchumi na kifedha," amesema Waziri wa Sheria Alphonse Charles Wright.

"Ni lazima kufungua uchunguzi wa kisheria ili kubaini chanzo cha fedha za akaunti hizi mbalimbali bila kuathiri hali ya kutofungia wakati inapoanzishwa kwa njia kinzani kwamba akaunti hizi hazihusiki na dhana zote za utakatishaji fedha," ameongeza.

Wanajeshi waliochukua mamlaka kwa nguvu mnamo Septemba 5, 2021 wamefanya vita dhidi ya ufisadi nchini Guinea kuwa mojawapo ya vita vyao vikuu vilivyotangazwa. Maafisa kadhaa wa zamani wanazuiliwa kwa makosa kama haya, wakiwemo waliotajwa kwenye barua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.