Pata taarifa kuu
GUINEA

Rais wa zamani wa Guinea Alpha Conde kufunguliwa mashtaka

Serikali ya kijeshi nchini Guinea, imetangaza kuwa, itamfungulia kesi ya mauaji aliyekuwa rais Alpha Conde, aliyeondolewa madarakani na jeshi mwezi Septemba mwaka uliopita.

Rais wa zamani wa Guinea Alpha Conde
Rais wa zamani wa Guinea Alpha Conde AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Conde mwenye umri wa miaka 84, ni miongoni mwa waliokuwa maafisa wakuu serikali wapatao 27 ambao sasa watafikishwa Mahakmani kujibu mashtaka ya mauaji na makosa mengine jinai kwa mujibu wa kiongozi wa mashtaka Alphonse Charles Wright.

Wanatuhumiwa mwa kuhusika pia kwa kuwazuia wapinzani wao kwa nguvu walipokuwa madatakani, utesaji, utekaji, wizi na ubakaji.

Ofisi ya kiongozi wa mashtaka, imesema, hatua hii imekuja baada ya kupokea malalamishi kutoka ka vuguvugu liloanzisha maandamano dhidi ya Conde, wakati akiwa rais.

Madai hayo yanaonekana kutekelezwa na uongozi wa rais huyo wa zamani, wakati wa kipindi chake cha mwisho cha miaka miwili, kabla hajaamua kuifayia marekebisho katiba, ili awanie tena uongozi wa nchi hiyo kwa muhula wa tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.