Pata taarifa kuu

Guinea: Utawala wa kijeshi wakubali kurejesha mamlaka kwa raia

Utawala wa kijshi nchini Guinea umekubali kurejesha mamlaka kwa raia baada ya miaka miwili, unasema waraka kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi uliyotolewa Ijumaa jioni (Oktoba 21). Ujumbe wa ECOWAS ulikuwa katika ziara ya kikazi mjini Conakry tangu Oktoba 16 ili kujadili kurejea kwa utaratibu wa kikatiba.

Kanali Doumbouya akiwa amezungukwa na wafuasi wa CRND. Septemba 17, 2021.
Kanali Doumbouya akiwa amezungukwa na wafuasi wa CRND. Septemba 17, 2021. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Wataalamu kutoka ECOWAS - waliokuwa katika ziara ya kikazi mjini Conakry tangu Jumapili - na wale kutoka nchini Guinea kwa pamoja wameandaa ratiba madhubuti ya kipindi cha mpito kitakachodumu miezi 24, klingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka jumuiya hiyo ya kikanda.

ECOWAS imesimamisha shughuli zote za usaidizi na kifedha na Guinea na kutangaza kufungiwa kwa mali ya kifedha na kupiga marufuku baadhi ya viongozi kusafiri katika eneo la ECOWAS. Bila shaka Conakry imebadilisha mtindo wake ili kuepuka vikwazo vipya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.