Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Guinea: Watu kadhaa wajeruhiwa katika makabiliano kati ya waandamanaji na polisi

Muungano wa Kitaifa wa Kutetea Katiba (FNDC) uliitisha maandamano Alhamisi hii, Oktoba 20 huko Greater Conakry. Mashirika ya kiraia yanashutumu usimamizi wa mpito unaofanywa na utawala wa kijeshi. Haya ni maandamano ya kwanza kufanyika tangu Septemba 5. Ghasia zilizuka Jumatano jioni.

Afisa wa Polisi akiwakabili waandamanaji huko Conakry mnamo Julai 28, 2022.
Afisa wa Polisi akiwakabili waandamanaji huko Conakry mnamo Julai 28, 2022. AFP - CELLOU BINANI
Matangazo ya kibiashara

Mapigano yameripotiwa sehemu ya usiku kati ya vijana na vikosi vya usalama ambavyo vilitumwa kwa wingi asubuhi ya leo kwenye kwenye eneo la Prince lakini pia katika maeneo mengine ya kimkakati katika mji mkuu kama vile barabara kuu ya Fidel Castro inayopitia vitongoji vya kusini na hasa kwenye randabauti Tannerie ambapo maandamano hayo yaliyoitishwa na Muungano wa Kitaifa wa Kutetea Katiba (FNDC) yangeanzia. Hakuna waandamanaji walioonekana kwenye eneo la mkutano, ambalo lilikuwa chini ya ulinzi mkali. Gari la maji ya kuwasha na magari kadhaa ya vikosi vya usalama yaliegeshwa ili kuwazuia wananaharakati hao kujipanga upya.

Watano wamejeruhiwa kwa risasi

Shirika hilo, lililovunjwa mnamo mwezi Agosti, lilitoa maonyo kadhaa, likitoa wito kwa Conakry ​​​​kutochukua magari yake, likiomba maduka kufungwa ili kuepusha "tukio lolote baya". Asubuhi ya Alhamisi hii, hakukuwa na msongamano wa magari katika barabara zenye msongamano wa watu wengi katika mji mkuu wa Guinea.

FNDC imeripoti majeraha matano ya risasi, ikiwa ni pamoja na mtu mmoja akiwa katika hali mbaya. Mtu huyo alipigwa risasi tumboni, katika wilaya ya Wanindara. Takwimu iliyotolewa na FNDC haiwezi kuthibitishwa kwa sasa, amebaini msemaji wa Wizara ya Usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.