Pata taarifa kuu

Félix Tshisekedi ateuliwa kuwa mpatanishi mzozo wa Chad

Siku tano baada ya ukandamizaji wa umwagaji damu dhidi ya maandamano yaliyosababisha vifo vya takriban watu 50 na wengine 300 kujeruhiwa nchini Chad, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (ECCAS) ilifanya mkutano wa kilele wa kipekee kuhusu suala hilo mjini Kinshasa siku ya Jumanne.

Félix Tshisekedi (hapa, ilikuwa Kinshasa mnamo Februari 20, 2022) atakuwa na dhamira ya kurejesha uaminifu kati ya pande tofauti kwenye mzozo nchini Chad.
Félix Tshisekedi (hapa, ilikuwa Kinshasa mnamo Februari 20, 2022) atakuwa na dhamira ya kurejesha uaminifu kati ya pande tofauti kwenye mzozo nchini Chad. © Arsène Mpiana / AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi watatu wa nchi waliitikia mwaliko wa Félix Tshisekedi, ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa ECCAS: Mahamat Idriss Déby wa Chad, Denis Sassou-Nguesso wa Kongo na Faustin-Archange Touadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Viongozi walioshiriki kikao hicho mjini Kinshasa walionyesha mshikamano wao na watu wa Chad. Walikaa kimya kwa dakika moja kuwakumbuka watu waliopoteza maisha yao. Bila kulenga mhusika hasa, walishutumu matumizi ya ghasia kwa malengo ya kisiasa.

Wakionyesha msimamo wao usioegemea upande wowote, viongozi wa hao wa kikanda waliwapongeza raia wa Chad kwa kuandaa mazungumzo ya kitaifa ambayo, wanasema, yaliweza kuleta pamoja vyama vingi vya kisiasa, makundi ya kisiasa na yale yenye silaha na mashirika ya kiraia.

Jumuiya hiyo inasema inataka kuchukua jukumu muhimu katika kipindi hiki cha mpito cha miaka miwili. Hivyo, Felix Tshisekedi aliteuliwa kuwa mpatanishi. Dhamira yake itakuwa kujenga tena uaminifu kati ya pande tofauti kwenye mzozo. Atasaidiwa katika nafasi yake na watu wawili, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Kongo wa Ushirikiano wa Kikanda na Rais wa Tume ya ECCAS, Gilberto Da Piedade Verissimo wa Angola. Wawili hawa wa mwisho wameteuliwa rasmi kuwa wajumbe maalum wa mpatanishi.

ECCAS inabaini kwamba sasa si wakati wa kuitenga Chad. Inaomba hata Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuimarisha msaada wao wa kidiplomasia, kifedha, vifaa na msaada wa kiufundi kwa mchakato wa mpito katika nchi hii.

Baadhi ya wapinzani wa Chad walitarajia kwamba ECCAS ingemchukulia vikwazo Mahamat Idriss Déby. Kwa mfano kwamba viongozi wa kanda hiyo wangelaani waziwazi vifo vilivyoripotiwa katika maandamano ya hivi majuzi. Ilikuwa pia nia ya vuguvugu la kiraia nchini DRC,  LUCHA, ambalo lilitoa taarifa kabla ya mkutano huo. LUCHA ilitoa wito kwa wajumbe wa ECCAS kulaani waziwazi kile ilichokiita mauaji ya Oktoba 20 na kutaka kukabidhiwa mamlaka kwa raia.

Mbele ya viongozi wenzake na wawakilishi wa nchi za ECCAS, Félix Tshisekedi alitoa picha ya kusikitisha ya hali ilivyo nchini Chad: "Ni wazi, makubaliano haya yanaonekana kusambaratika na maandamano yameanza tena hivyo kusababisha vifo vya watu wengi. Hali ya iliharibika ghafla. Matumaini ya kufanywa upya kwa demokrasia nchini Chad, baada ya maridhiano ya kitaifa, yamedidimia. "

Félix Tshisekedi pia anajua kwamba watu wa Chad wana hamu ya kurejesha amani na utulivu: "Wakati sio tena wa hotuba, lakini ni wa hatua madhubuti na za haraka kusaidia nchi hii ndugu kutekeleza mchakato huu kwa mafanikio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.