Pata taarifa kuu

Chad: Utulivu warejea na waandamanaji wasakwa baada ya vifo kuripotiwa

Baada ya maandamano katika mji mkuu wa Chad,  Ndjamena, na katika miji mingine ya nchi, utulivu umerejea Ijumaa hii, Oktoba 21 nchini humo. Hata hivyo, mamlaka inaendelea kuwakamata watu wanaoshukiwa kushiriki maandamano hayo siku ya Alhamisi.

Maafisa wa polisi wanashika doria, huko Moundou, Chad, Oktoba 20, 2022.
Maafisa wa polisi wanashika doria, huko Moundou, Chad, Oktoba 20, 2022. HYACINTHE NDOLENODJI via REUTERS - HYACINTHE NDOLENODJI
Matangazo ya kibiashara

Utulivu umerejea nchini Chad mbali na vida vichache vya mivutano Ijumaa asubuhi katika miji ya Ndjamena na Moundou. Shughuli zimerejea tena, baadhi yabarabara zimesafishwa. 

Ikumbukwe kwamba "operesheni ya kuwasaka waandamanaji" ilifanyika katika vitongoji ambapo maandamano yalifanyika. 

Maafisa wa polisi waliingia nyumba moja baada ya nyingine katika miji ya Ndjamena na Moundou ili kuwahoji waandamanaji wowote waliokuwa wametambuliwa. Makumi wamekamatwa kando ya maandamano, lakini hakuna taarifa kuhusu hatima ya wale waliokamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.