Pata taarifa kuu

Maandamano nchini Chad: Jumuiya ya Afrika ya Kati yakutana Kinshasa

Wakati Chad ikipata nafuu baada ya ukandamizaji mkali dhidi ya maandamano, Kinshasa inaandaa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika ya Kati (ECCAS) Jumanne (25 Oktoba) kuhusu hali ya kisiasa nchini humo. 

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati imetuma ujumbe kwa Chad baada ya ukandamizaji mbaya dhidi ya maandamano, hapa ni katika mji wa Ndjamena mnamo Oktoba 20, 2022.
Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati imetuma ujumbe kwa Chad baada ya ukandamizaji mbaya dhidi ya maandamano, hapa ni katika mji wa Ndjamena mnamo Oktoba 20, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Nchi 11 zitawakilishwa katika mkutano wa ana kwa ana uliyoitishwa na Félix Tshisekedi, rais wa sasa wa jumuiya hiyo. Wakati Ndjamena inataka kupata uungwaji mkono wa ECCAS, ECCAS inatafuta zaidi ya yote kuteua mpatanishi wa mgogoro huo.

Rais wa mpito wa Chad Mahamat Idriss Déby Itno anahudhuri mkutano huo mjini Kinshasa leo Jumanne katika mkutano wa kilele usio wa kawaida wa ECCAS, kuomba kanda ya Afrika ya Kati kuungwa mkono na kuisaidia kwa kipindi kizima cha mpito.

Matamshi hayo yanatoka kwa wanadiplomasia wa ngazi za juu wa Chad ambao wanakiri kwamba mauaji ya Oktoba 20 ni mambo mapya ambayo yatakuwa na uzito katika hitimisho la wakuu wa nchi katika mkutano huo. Rais wa mpito atalazimika kujitetea kwa matukio haya ambayo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua hamsini na zaidi ya 300 kujeruhiwa, anaripoti mwandishi wetu wa Ndjamena, Madjiasra Nako.

"Ni jibu la mapinduzi, uasi," wanasema maafisa wa Chad, ambao wana nia ya kutafuta kuungwa mkono na nchi jirani wakati wa mazungumzo. Mamlaka ya Chad pia inatumai kuwa uungwaji mkono kutoka kanda hiyo ndogo utawaruhusu kuepuka vikwazo kutoka Umoja wa Afrika.

Mkutano mfupi wa faragha

Mkutano huo hautadumu kwa muda mrefu, duru katika ofisi ya rais wa Kongo zinamwambia mwandishi wetu mjini Kinshasa, Patient Ligodi. Kazi hiyo itafanyika kwa siri, kukiwa na changamoto ya kufikia uteuzi wa mpatanishi wa ECCAS, inasema ofisi ya rais wa Kongo.

Marais wa Kongo-Brazzaville Denis Sassou-Nguesso na wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin Archange Touadéra pia wamethibitisha kuhudhuria kwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.