Pata taarifa kuu

Chad: Watu kadhaa wauawa wakati wa maandamano dhidi ya madaraka ya Mahamat Déby

Makabiliano makali yametokea Ndjamena na Moundou, mji wa pili nchini humo, kati ya maafisa wa polisi na waandamanaji wanaopinga kuongezwa kwa kipindi cha mpito. Makabialiano haya yameanza mapema asubuhi, Alhamisi hii, Oktoba 20. Utulivu umerejea katika mji mkuu, lakini mamlaka ya jiji hilo haijamaliza kuhesabu raia wake waliopoteza maisha katika ghasia hizo.

Makabiliano kati ya waandamanaji na maaffis wa Polisi huko Ndjamena yaligharimu maisha ya watu kadhaa Alhamisi hii, Oktoba 20, 2022.
Makabiliano kati ya waandamanaji na maaffis wa Polisi huko Ndjamena yaligharimu maisha ya watu kadhaa Alhamisi hii, Oktoba 20, 2022. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya watu waliingia katika mitaa ya mji mkuu siku ya Alhamisi asubuhi, ingawa maandamano yalikuwa yamepigwa marufuku na mamlaka. Wanapinga kuendelea madarakani wa rais wa mpito, Mahamat Déby.

Asubuhi hii, moshi mweusi ulionekana katika mji mkuu, matairi yalichomwa moto, vizuizi viliwekwa. Makabiliano makali yaliripotiwa katika wilaya kadhaa za jiji hilo.

Maafisa wa Polisi na wanajeshi wametumwakuzima maandamano hayo katika miji hiyo. Milio ya risasi za moto bado zinasikika.

Katika eneo la tisa, pamoja na idadi kubwa ya maafisa wa Polisi, watu waliovalia kiraia kwenye magari yenye rangi nyeusi walionekana wakiwafyatulia risasi waandamanaji.

Wakati huu zoezi la utafitaji wa miili ya watu waliouawa linaendelea, anaripoti mwandishi wetu huko Ndjamena, Madjiasra Nako. Waliojeruhiwa wamepelekwa katika vituo vya afya ambavyo viko chini ya uangalizi wa hali ya juu. Katika hospitali ya Muungano, kwa mfano, ambapo kulionekana angalau maiti 7. Familia zilizokuja kuchukua maiti ya ndugu zao zilirushiwa gesi. Mwanahabari mmoja aliweza kuhesabu angalau maiti 18 katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali Kuu ya Taifa. Miongoni mwa waliofariki ni mwanahabari Oredjé Narcisse ambaye amekuwa anafanya kazi katika kituo cha redio cha CEFOD.

Mapigano pia yaliripotiwa huko Moundou, mji wa pili wa nchi hiyo, ulioko kusini mwa nchi.

Wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji hao. [...] Kuna majeraha mengi ya risasi, amesema mwanaharakati wa haki za Binadamu jiji Moundou.

Ufaransa inalaani vurugu hizi. Katika taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Paris inataja hasa matumizi ya silaha za maangamizi dhidi ya waandamanaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.