Pata taarifa kuu

Ethiopia: Mazungumzo ya amani kati ya Serikali na waasi wa Tigray yaanza

Jumatatu, Oktoba 24yalitarajia kuanza nchini Afrika Kusini mazungumzo yaliyosubiriwa kwa muda mrefu kuhusu vita nchini Ethiopia, na wajumbe kutoka Tigray na serikali kuu ya Ethiopia mjini Johannesburg tangu Jumapili katika hali tete.

Kabla ya mazungumzo kati ya waasi wa Tigray na maafisa wa serikali kuu ya Ethiopia, sehemu ya jamii ya Tigray wamekusanyika Pretoria, Afrika Kusini, kuandamana dhidi ya vita, hapa ilikuwa tarehe 12 Oktoba 2022.
Kabla ya mazungumzo kati ya waasi wa Tigray na maafisa wa serikali kuu ya Ethiopia, sehemu ya jamii ya Tigray wamekusanyika Pretoria, Afrika Kusini, kuandamana dhidi ya vita, hapa ilikuwa tarehe 12 Oktoba 2022. AP - Themba Hadebe
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la shirikisho linazidi kupata mafanikio huko Tigray na jumuiya ya kimataifa inaendelea kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano. Habari ndogo sana hadi sasa imefichwa juu ya mazungumzo haya, lakini matarajio ya mazungumzo haya hayajapunguza mvutano kwa njia yoyote.

Wakati wajumbe wa pande hizo mbili walikuwa wamewasili Afrika Kusini, siku ya Jumatatu rais wa serikali ya Tigray alitoa tamko la kusema maneno makali zaidi, kutoka mji mkuu wa jimbo hilo la Mekele. Debretsion Gebremichael alibaini kuwa "vikosi vya Ethiopia na Eritrea vitazikwa huko Tigray", na kwamba jimbo hilo litakuwa "makaburi ya majeshi ya wavamizi".

Kiongozi wa Tigray alithibitisha kwamba alitaka kusuluhisha mzozo huo kwa amani. Hata hivyo, iwapo mazungumzo hayo yatashindwa, "majeshi yetu yana uwezo wa kuwatetea raia wao", alisema Debretsion Gebremichael.

Kujiamini kwake kunatofautiana na hali ya kijeshi chini, ambapo vikosi vya Tigray vimeanza kurejea nyuma. Katika siku za hivi karibuni, jeshi la shirikisho la Ethiopia limetangaza kuwa limerejesha udhibiti wake katika miji ya Alamata, Korem na hata Shire, eneo muhimu katika eneo hilo ambalo lina uwanja wa ndege.

Kulingana na vyombo vya habari vya Tigray, mashambulizi ya angani ya ndege zisizo na rubani yanaendelea, licha ya mazungumzo mjini Johannesburg, na mashambulizi huko Mekele, Maykinetal, Werkamba, Sele na Abiy Adi tangu Jumapili.

Hali inayotia wasiwasi jumuiya ya kimataifa. Kwa siku nyingi, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na hata Marekani zimekuwa zikitoa wito wa kusitishwa kwa uhasama. Hata hivyo, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield ametishi kuchukuliwa vikwazo: "Tuko tayari kuchukua hatua zinazofaa dhidi ya wale wanaozuia utatuzi wa mzozo," amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.