Pata taarifa kuu

Tigray: Washington yasitisha kuwafukuza wahamiaji wa Ethiopia

Marekani ilitangaza siku ya Ijumaa kwamba itawapa Waethiopia wote waliopo kwenye ardhi yake hadhi inayowalinda dhidi ya kufukuzwa na kuwaruhusu kufanya kazi, kwa sababu ya "mzozo wa silaha" na "mgogoro wa kibinadamu" katika nchi yao. Waethiopia hawajawahi kunufaika na hadhi hii, tofauti na Wasudan.

Hali inaendelea kutisha nchini Ethiopia, hasa katika jimbo la Tigray.
Hali inaendelea kutisha nchini Ethiopia, hasa katika jimbo la Tigray. © via REUTERS - WORLD FOOD PROGRAMME
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Usalama wa Ndani Alejandro Mayorkas alisema hawawezi kurejeshwa nchini Ethiopia kwa sababu ya "vurugu" lakini pia "uhaba mkubwa wa chakula, mafuriko, ukame na watu kuhama makazi yao".

Hadhi hii inayoitwa "ulinzi wa muda", iliyotolewa kwa muda wa miezi 18, inatumika kwa Waethiopia wote waliopo sasa katika ardhi ya Marekani na katika hali isiyo ya kawaida, lakini sio kwa wale ambao wataingia katika siku zijazo.

Takriban watu 26,700 wanahusika na hadhi hiyo, kulingana na Wizara ya Usalama wa Nchi.

Lakini hali inaendelea kuwa mbaya nchini mwao, ambapo vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya serikali ya Ethiopia ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed dhidi ya mamlaka ya waasi huko Tigray tangu Novemba 2020. Baada ya mapatano ya miezi mitano, mapigano yalianza tena mwishoni mwa mwezi Agosti kaskazini mwa Ethiopia.

Pande zote mbili, hata hivyo, zimeahidi kushiriki katika mazungumzo siku ya Jumatatu nchini Afrika Kusini chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika (AU).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.