Pata taarifa kuu

Mzozo nchini Ethiopia: Baraza la Amani na Usalama la AU lakutana

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) linakutana Ijumaa, kwa mara ya kwanza tangu kuanza tena kwa mapigano mwishoni mwa mwezi Agosti huko Tigray, kaskazini mwa Ethiopia, ili kufahamishwa kuhusu mchakato wa upatanishi unaoongozwa na jumuiya ya Afrika nzima.

Mauaji ya kikabila magharibi mwa Tigray yanatokea kutokana na mzozo kati ya serikali ya Ethiopia na chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF). Kwenye, kifaru cha jeshi kilichoharibika karibu na mji wa Humera mnamo Machi 3, 2021.
Mauaji ya kikabila magharibi mwa Tigray yanatokea kutokana na mzozo kati ya serikali ya Ethiopia na chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF). Kwenye, kifaru cha jeshi kilichoharibika karibu na mji wa Humera mnamo Machi 3, 2021. © REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Mwakilishi Mkuu wa AU katika Pembe ya Afrika, Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, ambaye anaongoza juhudi za upatanishi, anatarajiwa kuzungumza kwenye mkutano wa mtandaoni ambao ulipaswa kuanza asubuhi, kulingana na ratiba fupi iliyochapishwa na AU. 

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia linatazamiwa kukutana Ijumaa kujadili hali ya Ethiopia, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price amesema mjini Washington.

Serikali ya shirikisho ya Ethiopia, ambayo imekuwa katika mzozo mbaya wa silaha tangu Novemba 2020 na mamlaka ya waasi katika eneo la Tigray, ilitangaza Alhamisi kuwa imealikwa na AU kwenye mazungumzo ya amani mnamo Oktoba 24 nchini Afrika Kusini.

Si AU - yenye makao yake makuu mjini Addis Ababa - wala Pretoria hadi sasa hazithibitisha kufanyika kwa mazungumzo hayo siku ya Jumatatu. Mazungumzo ya awali, yaliyoitishwa na Umoja wa Afrika mapema mwezi Oktoba nchini Afrika Kusini, yalivurugika kabla hata hayajaanza.

Mjumbe maalum wa Marekani katika Pembe ya Afrika, Mike Hammer, amekuwa Addis Ababa kwa siku kadhaa "ambapo anaunga mkono juhudi za AU kuanzisha mazungumzo" ambayo Washington "inataka kuona yanaanza haraka iwezekanavyo", kulingana na Bw Price. Bwana Hammer "anawasiliana mara kwa mara na pande zinazohusika katika mgogoro huo, hasa wale ambao wanajiandaa kushiriki katika upatanishi", ameongeza msemaji wa wa Wizara ya mambo ya Nje ya Marekani.

Mapigano yalianza tena tarehe 24 Agosti kaskazini mwa Ethiopia, na kuhitimisha makubaliano ya miezi mitano na matumaini hafifu ya mazungumzo ambayo yalikuwa yameanza. Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Marekani hasa, walielezea wasiwasi wao katika siku za hivi karibuni kuhusu kushadidi kwa mapigano huko Tigray, jimbo linalosakamwa na mashambulizi ya majeshi ya shirikisho ya Ethiopia, yanayoungwa mkono kaskazini na jeshi la Eritrea - nchi ambayo inapakana kwenye mpaka wa kaskazini na jimbo la Tigray - na kusini na askari kutoka majimbo jirani ya Ethiopia.

Siku ya Jumatatu Vvikosi vya Ethiopia na Eritrea vilivamia na kudhibiti siku ya Jumatatu, baada ya siku kadhaa za mashambulizi ya angani, Shire, moja ya miji mikuu ya Tigray, ikiwa na karibu wakaazi 100,000 kabla ya vita na ambayo iliwapa hifadhi watu wengi waliokimbia makazi yao kutokana na vita.

Katika mazungumzo ya simu Jumatano na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema "ana wasiwasi sana" na "hatari ya ukatili mkubwa" kaskazini mwa Ethiopia. Siku ya Jumatatu, Bw. Guterres alisema hali nchini Ethiopia "imeshindwa kudhibitiwa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.