Pata taarifa kuu

Ethiopia: Waasi wa Tigray kushiriki katika mazungumzo ya amani nchini Afrika Kusini

Mamlaka ya waasi katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia ilitangaza siku ya Ijumaa (tarehe 21 Oktoba) kwamba watashiriki katika mazungumzo ya amani na serikali ya shirikisho ya Addis Ababa. Mazungumzo haya yanatarajiwa kufunguliwa Jumatatu, Oktoba 24 nchini Afrika Kusini chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika.

Wapiganaji wa vikosi vya waasi wa Tigray nchini Ethiopia, Juni 2021.
Wapiganaji wa vikosi vya waasi wa Tigray nchini Ethiopia, Juni 2021. AFP - YASUYOSHI CHIBA
Matangazo ya kibiashara

Lengo la mazungumzo haya itakuwa kujaribu kumaliza mzozo mbaya uliozuka tangu Novemba 2020, kati ya vikosi vya waasi wa Tigraya na jeshi la shirikisho la Ethiopia, linaloungwa mkono na jeshi la Eritrea. "Wajumbe wetu watakuwepo" Jumatatu nchini Afrika Kusini, alisema Ijumaa, Oktoba 21, mmoja wa wasemaji wa waasi wa Tigray, Kindeya Gebrehiwot.

Kwa upande wake, serikali ya shirikisho ya Ethiopia ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed imetangaza ushiriki wake katika mazungumzo haya ya amani ambayo yanaibua matumaini makubwa kimataifa. Mtu wa mwisho kuzungumza hadharani juu ya suala hilo, Ijumaa, Oktoba 21, mwishoni mwa mkutano uliofungwa wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ni Mmarekani Linda Thomas-Greenfield, mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa. "Hali nchini Ethiopia inazidi kuzorota. Kiwango cha mapigano haya na idadi ya vifo ni sawa na vile tunavuoona kwa sasa nchini Ukraine. Raia wasio na hatia wanakwama katika mapigano hayo. Katika miaka miwili ya vita, hadi watu nusu milioni wamepoteza maisha. Marekani ina wasiwasi mkubwa juu ya uwezekano wa ukatili mpya wa watu wengi.

Mapigano yameongezeka katika siku za hivi karibuni huko Tigray. Jeshi la Ethiopia, likisaidiwa na vikosi vya Eritrea, liliteka Shire, mojawapo ya miji mikuu katika eneo hilo, siku ya Jumatatu, baada ya siku kadhaa za mashambulizi ya angani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.