Pata taarifa kuu

Saleh Kebzabo, mpinzani wa hayati Idriss Déby, ateuliwa kuwa Waziri Mkuu

Saleh Kebzabo, mpinzani wa kihistoria wa Rais Idriss Déby Itno aliyeuawa mwaka 2021, ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Chad Jumatano kwa agizo la Mahamat Idriss Déby Itno, aliyetangazwa kuwa rais baada ya kifo cha baba yake na hivi karibuni aliongzwa kushikilia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka miwili.

Saleh Kebzabo, mpinzani wa kihistoria nchini Chad.
Saleh Kebzabo, mpinzani wa kihistoria nchini Chad. © Marco Longari/AFP
Matangazo ya kibiashara

Bw. Kebzabo, 75, mwandishi wa habari wa zamani, mgombea urais mara nne dhidi ya hayati Marshal Déby, na ambaye chama chake kilijiunga na serikali iliyoteuliwa na utawala wa kijeshi inayoongozwa na Jenerali kijana Mahamat Déby miezi 18 iliyopita, "ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu," kulingana na agizo lililotiwa saini na mkuu wa nchi.

Mnamo Aprili 20, 2021, wakati kilipotangazwa kifo cha Marshal Déby, aliyeuawa na waasi wakati akielekea vitani, jeshi lilimtangaza mtoto wake Jenerali Mahamat Déby, 37, kuwa rais wa Jamhuri katika kundi la majenerali 15, kwa kipindi cha mpito cha miezi 18 na kala ya uchaguzi "huru na wa kidemokrasia".

Lakini siku ya Jumatatu, aliapishwa tena kama mkuu wa nchi kwa kipindi cha mpito cha miaka miwili, kwa pendekezo la mazungumzo ya Kitaifa yanayopaswa kuleta pamoja wadau wote wa kisiasa nchini Chad pamoja na waasi, lakini yalisusiwa na vyama vingi vya upinzani wa kisiasa na makundi yenye silaha. Mahamat Déby aliahidi Jumatatu kuteua "katika siku chache zijazo" "serikali ya umoja wa kitaifa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.