Pata taarifa kuu

Burkina Faso: Kapteni Ibrahim Traoré atawazwa rasmi kama rais wa kipindi cha mpito

Kapteni Ibrahim Traoré anakuwa rasmi rais wa kipindi cha mpito. Kiongozi wa mapinduzi ya pili chini ya kipindi cha mwaka mmoja ameapishwa Ijumaa hii, Oktoba 21 wakati wa hafla ya kutawazwa kwake.

Sherehe za kuapishwa kwa Kepteni Ibrahim Traoré, Oktoba 21, 2022.
Sherehe za kuapishwa kwa Kepteni Ibrahim Traoré, Oktoba 21, 2022. © YouTube/RTB (Capture d'écran)
Matangazo ya kibiashara

Mbali na viongozi wa kijeshi, kulikuwa na vikosi vya wanamgambo, viongozi wa kimila na kidini, wakuu wa taasisi na wageni maalum wa rais wa mpito. Mbele ya wajumbe wa Baraza la Katiba, Kapteni Ibrahim Traoré aliinua mkono wake wa kulia na kuapa kwa heshima yake kuhifadhi, kuheshimu, kuheshimisha na kutetea katiba, makubaliano ya mpito na sheria. Kufanya kila linalowezekana kuhakikisha haki kwa wakazi wote wa Burkina Faso.

Kuzorota kwa hali ya usalama

Baada ya kutawazwa, Kaimu mkuu wa Baraza la Katiba alikumbusha sababu zilizotolewa za kufanya mapinduzi hayo, ni kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama na mamlaka iliyo kuwepo kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na hali hiyo. "Ni juu yako sasa kufanya kazi ili kuiondoa Burkina Faso kutoka katika hali ambazo zimekuwa msingi wa kukosekana kwa utulivu kuanzia kwenye uongozi wa serikali kwa muongo mmoja," amesema Kaimu Mkuu wa Baraza la Katiba.

'Nitapigana hadi pumzi ya mwisho'

Rais wa mpito amehutubia wananchi wake kwa hotuba ya mdomo bila maandishi. Kulingana na Kapteni Ibrahim Traoré, vikosi vya jeshi vya Burkina Faso havikabiliwi na vita visivyo vya kawaida, lakini vinakabiliwa na jeshi lililojipanga vyema. "Malengo yetu ni kurejesha maeneo yanayokaliwa kwenye himaya yetu, kuwapumzisha wananchi wake wote wanaoteseka na kukuza maendeleo ," amekumbusha rais huyo wa mpito.

Amehakikisha kwamba ataweka ahadi zote zilizotolewa mbele ya marafiki na washirika wote wa Burkina Faso. "Hakuna hasara kubwa itakayotokea kwa kuiondoa Burkina Faso katika hali hii. Dira yetu itakuwa watu daima. Kwa taifa langu, nitapigana hadi pumzi ya mwisho,” amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.