Pata taarifa kuu

Waziri mkuu wa mpito wa Chad ajizulu

Waziri Mkuu wa Chad amejiuzulu Jumanne, siku moja baada ya tangazo la Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno, kuongeza miaka miwili kama rais wa kipindi cha "mpito", na amesema uteuzi ujao wa "serikali ya umoja wa kitaifa", alitangaza N' Djamena.

Albert Pahimi Padacke, Waziri Mkuu wa Chad (wakati huo Waziri wa Mambo ya Nje) wakati wa mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Ahmad Allam-Mi (hayupo pichani) Februari 22, 2008 mjini Paris.
Albert Pahimi Padacke, Waziri Mkuu wa Chad (wakati huo Waziri wa Mambo ya Nje) wakati wa mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Ahmad Allam-Mi (hayupo pichani) Februari 22, 2008 mjini Paris. © MEHDI FEDOUACH/AFP
Matangazo ya kibiashara

Albert Pahimi Padacé aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwake kwa serikali yake wakati wa mazunguzo na mkuu wa nchi, ambaye alikubali kuachia ngai, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka ikulu ya  rais. Aliteuliwa miezi 18 iliyopita na Mahamat Déby.

Jumatatu, rais huyo alitawazwa, kwa kipindi kipya cha miaka miwili ya mpito kuelekea "uchaguzi huru na wa kidemokrasia", ambao alikuwa ameahidi miezi 18 iliyopita.

Mnamo Aprili 20, 2021, jeshi la kijeshi la majenerali 15 lilimpeleka hadi mkuu wa nchi hii kubwa ya Sahelia siku moja baada ya kifo cha baba yake Idriss Déby Itno, aliyeuawa mbele ya waasi baada ya kutawala kwa miaka 30 bila kupingwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.