Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Chad: Idadi ya vifo kufuatia makabiliano kati ya wafugaji na wakulima yaongezeka hadi 19

Watu 19 waliuawa katikati ya mwezi Septemba katika kipindi cha siku mbili za mapigano kati ya wafugaji na wakulima kusini mwa Chad, nchi ambayo mara kwa mara inakumbwa na migogoro mibaya kati ya jamii hizi za kuhamahama, kulingana na ripoti mpya kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka iliyotolewa leo Jumanne.

Makabiliano kati ya watu wawili kutoka jamii hizi mbili katika eneo la Marabe, kijiji kidogo kilicho kilomita 500 kusini mashariki mwa mji mkuu N'Djamena, yaligeuka na kuwa mapigano ya siku mbili ambayo yalienea katika maeneo mawili jirani mnamo Septemba 13 na 14 na idadi ya vifo vya watu 10 imetangazwa.
Makabiliano kati ya watu wawili kutoka jamii hizi mbili katika eneo la Marabe, kijiji kidogo kilicho kilomita 500 kusini mashariki mwa mji mkuu N'Djamena, yaligeuka na kuwa mapigano ya siku mbili ambayo yalienea katika maeneo mawili jirani mnamo Septemba 13 na 14 na idadi ya vifo vya watu 10 imetangazwa. © Sayouba Traoré/RFI
Matangazo ya kibiashara

Vurugu hizi kati ya jamii zinatokea mara kwa mara katikati na kusini mwa Chad, ambako wakazi wengi wana silaha. Makabiliano hayo ni kati ya wafugaji wahamaji wa Kiarabu na wakulima wa kiasili, ambao wanawashutumu wafugaji hao kwa kupora mashamba yao kwa minajili ya malisho ya mifugo yao.

Makabiliano kati ya watu wawili kutoka jamii hizi mbili katika eneo la Marabe, kijiji kidogo kilicho kilomita 500 kusini mashariki mwa mji mkuu N'Djamena, yaligeuka na kuwa mapigano ya siku mbili ambayo yalienea katika maeneo mawili jirani mnamo Septemba 13 na 14 na idadi ya vifo vya watu 10 imetangazwa.

"Watu kumi na tisa waliuawa, 22 kujeruhiwa na 18 kukamatwa," Lamane Nguessangar, mwendesha mashtaka wa umma katika mahakama ya rufaa ya Sahr, mji mkuu wa jimbo la Moyen-Chari, ameliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu.

Utulivu ulirejea baada ya siku mbili vikosi vya usalama kuingilia kati, mamlaka ya eneo hilo ilisema wakati huo.

Mabedui hao kwa ujumla hutoka katika maeneo kame ya Sahel kaskazini mwa Chad na kutafuta kuishi kwenye ardhi yenye rutuba zaidi ambayo hufaa kwa ufugaji wa ngamia na kondoo wao hasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.