Pata taarifa kuu

ECOWAS yatangaza vikwazo dhidi ya utawala wa kijeshi wa Guinea

Katika mkutano usio kuwa wa kawaida wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, uliofanyika Alhamisi jioni Septemba 22 huko New York, kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi waliamua kuchukua "vikwazo vya maendeleo" dhidi ya utawala wa kijeshi nchini Guinea ambao hautaki kuheshimu kipindi kilichotolewa na jumuiya hiyokuhusu kukabihi madaraka raia.

Kiti cha mwakilishi wa Guinea kiko tupu katika kikao cha ECOWAS, Septemba 16, 2021.
Kiti cha mwakilishi wa Guinea kiko tupu katika kikao cha ECOWAS, Septemba 16, 2021. © NIPAH DENNIS/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mpango wa ofisi ya rais wa Guinea-Bissau, waliamua pia kutuma ujumbe Bamako kukutana na mamlaka ya Mali.

Mwenyekiti wa Tume ya ECOWAS, Omar Alieu Touray wa Gambia, ndiye ambaye alifahamisha waandishi wa habari, wakati wakuu wa nchi na mawaziri waliondoka. jengo hilo bila neno na viti vitatu vikiwa tupu, vkile cha Burkina Faso, Mali na Guinea, vilivyosimamishwa kutoka kwa ECOWAS, anaripoti mjumbe wetu maalum huko New York, Léonard vincent.

Hitimisho la mkutano huo usio kuwa wa kawaida, liko katika nukta mbili. Kwanza, "tumeamua kuchukua vikwazo dhidi ya Guinea", ametangaza mwenekiti wa Tume ya ECOWAS. Kulingana na waraka unaoemezea kwa kifupi mkutano huu wa wakuu wa nchi, "iliamuliwa kuchukua vikwazo vya kimaendeleo kwa watu binafsi na dhidi ya utawala wa kijeshi nchini Guinea". "Haraka sana, rais wa sasa wa ECOWAS na rais wa Tume ya ECOWAS watatengeneza orodha ya watu watakaoidhinishwa na, hatua kwa hatua, kutekeleza vikwazo hivi", kulingana na nakala hii.

Kwa mujibu wa onyo lililotolewa kwenye mkutano wa kilele wa Accra mnamo Julai 3, mabalozi wa ECOWAS huko Conakry "wanaitwa tena kwa mashauriano", "msaada wa kifedha na shughuli za taasisi za kifedha" za ECOWAS zimesimamishwa. Mali ya kifedha serikali na ya wanachama wa utawala wa kijeshi, zimesizuiwa, na ni marufuku kusafiri.

Mamlaka ya mpito ya Guinea hatimaye inatolewa wito kukubali, ndani ya "mwezi mmoja", kipindi cha mpito "kinachokubalika", bila maelezo zaidi, chini ya adhabu ya vikwazo vipya "vikali zaidi". Kwa hivyo haya ni maelewano: tunajua kwamba baadhi ya wakuu wa nchi waliomba hatua kali na za haraka zaidi dhidi ya Conakry, huku wengine wakiegemea kwenye maamuzi "ya kimaendeleo".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.