Pata taarifa kuu

Guinea: Utawala wa kijeshi wataja "aibu" na "uongo" maneno ya rais wa ECOWAS

Utawala wa kijeshi nchini Guinea unamshtumu rais wa sasa wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, muda mfupi kabla ya mkutano wa kilele wa jumuiya hii ya kikanda, ikikashifu matamshi yaliyotolewa Jumatano kama "aibu" na kumshutumu kwa kutekeleza diplomasia ya "kibaraka".

Katika video iliyotumwa kwenye mtandao wa Facebook mnamo Septemba 22, 2022, Kanali Amara Camara alikashifu maoni ya Umaro Sissoco Embalo katika mahojiano na RFI na France 24.
Katika video iliyotumwa kwenye mtandao wa Facebook mnamo Septemba 22, 2022, Kanali Amara Camara alikashifu maoni ya Umaro Sissoco Embalo katika mahojiano na RFI na France 24. © Facebook/Présidence de la République de Guinée
Matangazo ya kibiashara

"Uongo na matamshi machafu ambayo yanafanana na vitisho siku hizi ni mazoea ya kurudisha nyuma ambayo hayaheshimu yule aliyoyatoa na wakati huo huo kuchafua sura ya ECOWAS. Hatuwezi kuvumilia aibu hii, "amesema Kanali Amara Camara, mmoja wa viongozi wa serikali na katibu mkuu wa ofisi ya rais wa Mpito, katika video iliyowekwa kwenye mtandao wa Facebook, ukurasa wa ofisi ya rais wa Guinea. "Hatuko katika uhusiano wa kibaraka au kufuata yale unayoambiwa" ameongeza.

Kanali Camara amemkosoa rais wa sasa wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embalo, kwenye taarifa zake alizotoa kwa RFI na France 24 siku ya Jumatano Septemba 22.

Mkutano wa kipekee wa kilele wa ECOWAS wapangwa kufanyika leo mjini New York

Rais Embalo alionya kwamba Guinea itakabiliwa na "vikwazo vizito" ikiwa utawala wa kijeshi uliyoingia madarakani kwa nguvu mnamo mwezi Septemba 2021 utaendelea kutaka kushikilia madaraka kwa miaka mitatu. Alithibitisha tena kwamba wakati wa ziara yake nchini Guinea alipata makubaliano na jeshi la serikali kutoa nafasi kwa raia waliochaguliwa baada ya miaka miwili, jambo ambalo Kanali Camara alilitaja kuwa "uongo".

Viongozi wa nchi wanachama wa ECOWAS wanatarajiwa kukutana kwa mkutano wa kilele siku ya Alhamisi alasiri mjini New York kando ya Mkutano Kuu wa Umoja wa Mataifa, huku hali nchini Guinea na mzozo kati ya Mali na Côte d'Ivoire vikiwekwa kwenye ajenda ya mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.