Pata taarifa kuu

Mamadi Doumbouya azuru Mali kabla ya mkutano muhimu wa ECOWAS

Kanali Mamadi Doumbouya alitua Jumatano alasiri kwenye uwanja wa ndege wa Bamako, mji mkuu wa Mali, Jumatano, Septemba 21, kwa ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu aingie madarakani Septemba 5, 2021. 

Kanali Mamadi Doumbouya, kiongozi mwenye nguvu Conakry. Septemba 10, 2021.
Kanali Mamadi Doumbouya, kiongozi mwenye nguvu Conakry. Septemba 10, 2021. REUTERS - SALIOU SAMB
Matangazo ya kibiashara

Alipokelewa na mwenzake wa Mali, Kanali Assimi Goïta. Hii nii katika muktadha mahususi wa kimataifa, kwani vikwazo vinaweza kuchukuliwa dhidi ya mamlaka ya Conakry wakati wa kikao cha kikao kisicho kuwa cha kawaida cha Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, kilichopangwa kufanyika leo Alhamisi huko New York, nchini Marekani.

Kabla ya kuondoka kwake, Kanali Mamadi Doumbouya aliwaambia waandishi wa habari madhumuni ya ziara yake: "Niko Bamako pamoja na kaka yangu, Rais Assimi Goïta, kusherehekea uhuru wa Mali na kuandamana na raia wa Mali, ambao ni ndugu. Leo Alhamisi, Mali inaadhimisha miaka 62 ya uhuru wake.

Mamadi Doumbouya alisema yuko pamoja na "ndugu zake wa Mali" kwa maadhimisho ya uhuru.

Kutoka Bamako, Kanali Doumbouya alitoa wito kwa wananchi wa Guinea kuungana na kuahidi kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa nchini Guinea.

Lakini ziara hii nchini Mali, ikiwa ni safari ya kwanza kwa mkuu wa serikali ya Guinea tangu alipompindua Rais Alpha Condé, inakuja katika mkesha wa kikao kisicho cha kawaida cha ECOWAS, kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York.

ECOWAS inaweza kuamua juu ya "vikwazo vikali" dhidi ya mamlaka ya Conakry ikiwa watadumisha kipindi chao cha mpito cha kijeshi cha miezi 36.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.