Pata taarifa kuu
ECOWAS

Viongozi wa ECOWAS kuamua hatima ya Mali, Burkina Faso na Guinea

Viongozi wa mataifa ya Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, wanakutana kesho, kuthathmini hatima ya vikwazo vya kiuchumi iliyowekea mataifa matatu, kufuatia hatua ya jeshi kuchukua madaraka.

Viongozi wa ECOWAS waliokutana kwenye mkutano uliopita, jijini Accra
Viongozi wa ECOWAS waliokutana kwenye mkutano uliopita, jijini Accra © nigeria vice president office
Matangazo ya kibiashara

Hatima ya nchi za Mali, Burkina Faso na Guinea ipo mikpnoni mwa viongozi w anchi hizo za Afrika Magharibi, watakaokutana jijini Accra nchini Ghana.

Mkutano huo utaamua iwapo vikwazo hivyo viendelee kuwepo au viondolewe, wakati huu wakiendelea kushinikiza uongozi wa kijeshi katika nchi hizo, kurejesha madaraka kwa raia, kwa kuandaa uchaguzi.

Mali ambayo jeshi limesema uchaguzi utafanyika mwaka 2024, imekuwa chini ya vikwazo hivyo tangu mwezi Januari, hali ambayo imetikisa uchumi wake.

Hata hivyo, Burkina Faso na Guinea zilisimamishwa wanachama wa ECOWAS, katika kipindi hiki ambacho pia, uongozi wa Jumuiya hiyo wamekuwa katika mazungumzo na uongozi wa kijeshi hasa nchini Mali, yakiongozwa na aliyekuwa rais wa Nigeria Goodluck Jonathan.

Uongozi wa Guinea hata hivyo, umekataa msuluhishi wa ECOWAS na kutangaza kurejesha uongozi kwa raia baada ya miezi 36, muda ambao Umoja wa Afrika unasema haukubaliki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.