Pata taarifa kuu

ECOWAS kukutana mjini New York kuhusu Mali na Guinea, chini ya tishio la 'vikwazo vikali'

Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za afrika Magharibi, ECOWAS,  uliokuwa unasubiriwa kwa hamu unafanyika Alhamisi, Septemba 22 huko New York, kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Mkutano huo ambao uliitishwa kwa mpango wa ofisi ya rais wa Guinea-Bissau, utajadili hali nchini Guinea na Mali, vyanzo vya mvutano kati ya jumuiya hii ya kikanda na nchi hizo mbili.

Rais wa Guinea-Bissau na rais wa sasa wa ECOWAS Umaro Sissoco Embalo, wakati wa mkutano wa mwisho wa jumuiya hiyo, mjini Accra Julai 3, 2022.
Rais wa Guinea-Bissau na rais wa sasa wa ECOWAS Umaro Sissoco Embalo, wakati wa mkutano wa mwisho wa jumuiya hiyo, mjini Accra Julai 3, 2022. © Nipah Dennis / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatimaye, mkutano wa kilele usio kuwa wa kawaida wa ECOWAS utakuwa tukio la Afrika la Mkutano huu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Mkutano ambao uliombwa na ofisi ya rais wa Guinea-Bissau na utafanyika katika jengo lililo karibu na Umoja wa Mataifa, baada ya ya alasiri.

Katika ajenda ya mkutano huo, kulingana na Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo: "kutathmini upya hali ya Guinea na Mali", chanzo cha mvutano kati ya jumuiya hiyo ya kikanda na miji nchi hizi mbili.

Kwa sababu ikiwa rais wa sasa wa ECOWAS ameelezea kuridhishwa kwake na mabadiliko nchini Burkina Faso - ambayo anasema "inaheshimu mapendekezo yaliyotolewa na ECOWAS - si sawa na mamlaka ya mpito nchini Guinea na Mali. Ndio maana alitaka mkutano huu wa uso kuwa wakawaida kufanyika huko New York.

"Vikwazo vikali" viko "mezani"

Hii itakuwa fursa kwa Rais wa zamani wa Benin Thomas Boni Yayi, mpatanishi wa ECOWAS, kuwajulisha Wakuu wa Nchi kuhusu kuhusu misheni yake ya hivi majuzi huko Conakry mwishoni mwa mwezi wa Agosti: atabainisha mambo ya makubaliano na yale ambayo hawakuweza kukubaliana na mamlaka ya mpito ya Guinea na kutoa mapendekezo kwa Conakry na kwa nchi Wanachama.

Pointi kuu ambazo hawakukubaliana ni muda wa mpito. Rais Embalo, anasema miezi 24 walioafikiana "haiwezi kujadiliwa" na kuna uwezekano "vikwazo vikali" kuchukuliwa.

Kuhusiana na Mali, suala ambalo hawakuafikiana ni lile la wanajeshi 46 wa Côte d’Ivoire wanaozuiliwa tangu Julai 10, ambao Côte d'Ivoire inaomba kuachiliwa mara moja. Lakini pia matumizi ya ratiba iliyoanzishwa mjini Accra mwezi Julai, wakati huo huo na kuondolewa kwa vikwazo vinavyoathiri Bamako na ambavyo "vitawezesha kufanyika kwa uchaguzi na kurejeshwa kwa utawala wa kiraia" ifikapo mwaka 2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.