Pata taarifa kuu
Guinea - Siasa

Guinea: Ujumbe wa ECOWAS kujadili kipindi cha mpito

Msuluhishi wa Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, rais wa zamani wa Benin, Thomas Boni Yayi yupo jijini Conakry, kujadili mchakato wa kukabidhi madaraka kutoka kwa jeshi kwenda kwa uongozi wa kiraia.

Kanali Doumbouya kiongozi wa kijeshi nchini Guinea  Septemba 17, 2021
Kanali Doumbouya kiongozi wa kijeshi nchini Guinea Septemba 17, 2021 AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Msuluhishi huyo wa ECOWAS amepanga kukutana na viongozi wa kijeshi nchini humo, ili kujadiliana kuhusu muda unaokubaliwa wa kukabidhi madaraka kwa uongozi wa kiraia.

ECOWAS imetoa mpaka Agosti kwa uongozi huo wa mpito kuweka wazi mipango yake, la sivyo itawekewa vikwazo.

Msuluhishi huyo amekwenda jijini Conankry na pendekezo la kumtaka kiongozi wa Kijeshi  Kanali Mamadi Doumbouya, kukubali mchakato wa miaka miwili utakaowezesha madaraka kurejea kwa raia, kwa kufanyika kwa uchaguzi.

Mbali na pendekezo hili, uongozi wa kijeshi pia unapendekeza kuwepo kwa mazungumzo ya kisiasa kati ya uongozi wa kijeshi na wanasiasa, lakini wanasiasa wakuu Sidya Touré na Cellou Dalein Diallo hawapo nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.