Pata taarifa kuu

Mali: Je, makubaliano yanawezekana na ECOWAS kuhusu chaguzi zijazo?

Mkutano wa kilele usio wa kawaida wa Wakuu wa Nchi za ECOWAS unafunguliwa kesho Jumamosi huko Accra, mji mkuu wa Ghana, ambao unashikilia uenyekiti wa Jumuiya hiyo ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi.

Kiti cha mwakilishi wa Mali katika makao makuu ya ECOWAS huko Accra (Ghana), Septemba 16, 2021.
Kiti cha mwakilishi wa Mali katika makao makuu ya ECOWAS huko Accra (Ghana), Septemba 16, 2021. © AFP - NIPAH DENNIS
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu utafuatiwa na mkutano wa wakuu wa nchi za UEMOA, Umoja wa Kiuchumi na Fedha wa Afrika Magharibi. Kwenye ajenda ya mazungumzo kutajadiliwa mabadiliko yanayoendelea katika nchi tatu ambazo hivi karibuni zimekumbwa na mapinduzi ya kijeshi: Guinea, Burkina, na zaidi ya yote Mali, ambayo inatarajia, wakati wa mkutano huu, kwa uwezekano wa kuondolewa kwa vikwazo vinavyoathiri nchi hiyo tangu mapema mwezi Januari. Kwa hili, makubaliano yatabidi kufikiwa kuhusu kufanyika kwa chaguzi zijazo ili kurejea kwa utaratibu wa kikatiba.

Utawala wa jeshi unaoongozwa na rais wa sasa wa mpito, Kanali Assimi Goïta, ulichukua mamlaka mwezi Agosti 2020, mwaka mmoja na miezi tisa iliyopita. Changamoto ya mkutano huu ni kujua ni lini mamlaka hii itarejeshwa kwa raia wa Mali. Baada ya kukata tamaa katika kuandaa uchaguzi wa rais na wabunge Februari mwaka jana, kama walivyoahidi hapo awali, mamlaka huko Bamako kwanza ilipendekeza kuongeza muda wa mpito kwa miaka mingine mitano.

Pendekezo hili ambalo linazingatiwa kuwa la uchochezi na nchi jirani za ECOWAS, hatimaye Bamako ilipendekeza kipindicha mpito kuongezwa kwa miaka minne, kisha miaka miwili ya ziada. Kwa upande wa Waziri Mkuu wa mpito Choguel Maïga, na wafuasi wote wa mamlaka ya sasa, haiwezekani tena kwenda chini ya kipoindi hii cha mikaa miwili. ECOWAS inaomba kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba ndani ya miezi kumi na sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.