Pata taarifa kuu

Tisa wafariki katika mapigano kati ya wafugaji na wakulima nchini Chad

Watu tisa waliuawa Ijumaa katika mapigano kati ya wakulima na wafugaji kilomita 500 kusini mwa N'Djamena, mji mkuu wa Chad, unaokumbwa na mzozo mbaya baina ya jamii, gavana wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu.

Mnamo Agosti 10, watu 13 waliuawa katika mapigano kati ya wakulima na wafugaji. Mgogoro huo ulianza kwa mkulima kuibiwa jembe na mtoto wa mfugaji.
Mnamo Agosti 10, watu 13 waliuawa katika mapigano kati ya wakulima na wafugaji. Mgogoro huo ulianza kwa mkulima kuibiwa jembe na mtoto wa mfugaji. © Sayouba Traoré/RFI
Matangazo ya kibiashara

Vurugu kati ya jamii hutokea mara kwa mara katikati na kusini mwa Chad, ambako wakazi wengi wana silaha. Mapigano hayo ni kati ya wafugaji wa kuhamahama wa Kiarabu na wakulima wa kiasili wasiofanya kazi ambao wanawashutumu wenzao hasa kwa kuharibu mashamba yao kwa ajili la malisho ya mifugo yao.

"Hatujui ni sababu gani za mapigano haya kati ya wakulima na wafugaji yaliyotokea Ijumaa karibu na Mengalang", kijiji kidogo kilichoko kusini mwa Chad, Abdelkerim Seïd Bauche, gavana wa Logone Mashariki, ameliambia shirika la habari la AFP, akibainisha kuwa " watu tisa waliuawa". "Hali sasa imedhibitiwa na vikosi vya ulinzi na usalama, ambavyo vimetumwa kwenye eneo la tukio," ameongeza Bw. Seid Bauche.

Mnamo Agosti 10, watu 13 waliuawa katika mapigano kati ya wakulima na wafugaji. Mgogoro huo ulianza kwa mkulima kuibiwa jembe na mtoto wa mfugaji.

Mnamo Agosti 2021, watu 22 waliuawa katika mapigano ya kijamii kilomita 200 mashariki mwa mji mkuu wa Chad. Mnamo mezi wa Februari 2021, watu 35 waliuawa kusini mwa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.