Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Kumi wauawa katika mapigano kati ya wafugaji na wakulima nchini Chad

Watu kumi wameuawa katika mapigano ya siku mbili kati ya wafugaji na wakulima kusini mwa Chad, nchi ambayo mara kwa mara inakumbwa na mizozo mikali kati ya jamii hizi za kuhamahama na wakulima wa kiasili, gavana wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi.

Mifugo la mmoja wa wafugaji wa Chad katika eneo la Ouaddaï, mashariki mwa Chad.
Mifugo la mmoja wa wafugaji wa Chad katika eneo la Ouaddaï, mashariki mwa Chad. AFP - AMAURY HAUCHARD
Matangazo ya kibiashara

Mapigano kati ya watu wawili kutoka jamii hizi katika kijiji cha Marabe, kijiji kidogo kilicho umbali wa kilomita 700 kusini mwa mji mkuu N'Djamena, ndiyo chanzo cha mapigano hayo siku ya Jumanne, ambayo yalienea hadi Jumatano katika vijiji viwili jirani, amesema Ali Ahmat Akhabache, gavana wa mkoa wa Moyen-Chari, mpakani na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

"Watu kumi waliuawa na ishirini walijeruhiwa," amesema na kuongeza: "vikosi vya usalama vilifanikiwa kurejesha hali ya utulivu na hali imedhibitiwa kabisa tangu jana," amebaini.

Mwezi Agosti, watu 22 waliuawa katika makabiliano kama hayo kati ya wakulima na wafugaji kilomita 500 kusini mwa N'Djamena.

Ukatili huu wa mara kwa mara kwa ujumla ni kati ya wafugaji wa kuhamahama wa Kiarabu na wakulima wa kiasili ambao wanawashutumu wafugaji hao kwa kuharibu mashamba yao kwa kuchunga mifugo yao.

Vurugu kati ya jamii hizi hutokea mara kwa mara katikati na kusini mwa nchi, ambapo wakazi wengi wana silaha.

Mabedui hao kwa ujumla hutoka katika maeneo kame ya Sahel kaskazini mwa Chad na wanataka kukaa kwenye ardhi yenye rutuba inayofaa kufuga ngamia na kondoo wao hasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.