Pata taarifa kuu
CHAD

Mazungumzo yaliyocheleweshwa yaanza nchini Chad

Mazungumzo yaliyocheleweshwa kuhusu nchi ya Chad yameanza leo, ikiwa ni hatua kubwa ya kihistoria kuhusu hatima ya nchi hiyo ya Afrika ya Kati, licha ya baadhi ya wanasiasa wa upinzani kususia.

Rais wa mpito wa Chad, Mahamat Idriss Deby akizindua sanamu ya amani, msamaha na maridhiano katika ikulu ya Januari 15 kwenye hafla ya ufunguzi wa mazungumzo ya kitaifa jumuishi, huko Ndjamena, Agosti 20, 2022.
Rais wa mpito wa Chad, Mahamat Idriss Deby akizindua sanamu ya amani, msamaha na maridhiano katika ikulu ya Januari 15 kwenye hafla ya ufunguzi wa mazungumzo ya kitaifa jumuishi, huko Ndjamena, Agosti 20, 2022. AFP - AURELIE BAZZARA-KIBANGULA
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wajumbe 1,400 kutoka uongozi wa kijeshi, mashirika ya kiraia na baadhi ya wanasiasa wa upinzani pamoja na muungano wa vyama vya Wafanyakazi, wamekutana jijini N'Djamena kushiriki kwenye mazungumzo hayo ya amani, ambayo yanatarajiwa kuendelea kwa wiki tatu zijazo.

Akifungua mazungumzo hayo, kiongozi wa kijeshi nchini humo Jenerali Mahamat Idriss Deby amesema, hatua hii ni muhimu kwa historia ya Chad kuunda nchi thabiti.

Mazungulzo haya yalikuwa yafanyike mwezi Februari jijini Doha, lakini yaliahirishwa kwa sababu ya makundi kadhaa yenye silaha kutoonesha nia ya kushiriki.

Hatima ya mazungumzo haya ni kuiwezesha Chad kuwa na uchaguzi huru na haki, baada ya kumalizika kwa uongozi wa kijeshi wa miezi 18.

Hata hivyo vuguguvu la upinzani FACT na muungano wa vyama vya upinzani Wakit Tamma, umekataa kushiriki kwenye mazungumzo haya kwa kile inachosema haina imani na uongozi wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.