Pata taarifa kuu

Chad: Bado mazungumzo hayajafaulu kando ya majadiliano ya kitaifa

Nchini Chad, kazi ya majadiliano shirikishi ya kitaifa imeanza tena Jumamosi hii, Septemba 3, baada ya kusimamishwa kwa siku tatu ili kujadiliana na vyama vya siasa na mashirika ya kiraia ambayo yameamua kususia. Kazi ilipoanza tena, baraza la mawaziri limegundua kuwa juhudi hizo hazijafaulu, huku vikosi vya usalama vikiendelea kuzingira makao makuu ya chama cha upinzani, Les Transformateurs. Chama hiki hakishiriki katika majadiliano haya.

Rais wa mpito wa Chad, Mahamat Idriss Deby (katikati) wakati wa sherehe za ufunguzi wa mazungumzo hayo, mjini N'Djamena, Chad, tarehe 20 Agosti 2022.
Rais wa mpito wa Chad, Mahamat Idriss Deby (katikati) wakati wa sherehe za ufunguzi wa mazungumzo hayo, mjini N'Djamena, Chad, tarehe 20 Agosti 2022. AFP - AURELIE BAZZARA-KIBANGULA
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kurejeshwa kwa shughuli za kongamano hilo, Jumamosi hii asubuhi, mratubu wa majadiliano hayo, Gali Ngoté Gata amekiri kwamba siku tatu za kusimamishwa kwa majadiliano haya ya kitaifa hazikufanya iwezekane kushawishi chama hiki kuingia tena kwenye mazungumzo.

Viongozi wa kidini na wazee ambao ni wajumbe katika kamati ya upatanishi wa dharura pia wamekataa kuwa sehemu ya mazungumzo. Uongozi ulizingatia uamuzi wao huku ukiwataka waendelee na juhudi zao.

Aidha, rasimu ya ajenda kuhusu uendeshaji wa kongamano hilo hadi mwisho wake, iliyopangwa Jumatatu, Oktoba 5, ilisambazwa kwa washiriki. Itachunguzwa Jumatatu katika kikao.

Wakati huo huo, makao makuu ya chama cha Les Transformateurs bado yamezingirwa na vikosi vya usalama. Wanaharakati wachache, hata hivyo, walijaribu kufika karibu na makao makuu ya chama cha Succes Masra. Walifukuzwa na mabomu ya machozi.

Katika video iliyowekwa kwenye mtandao wa Facebook, kiongozi wa Transformateurs alisema amepokea kutoka kwa serikali pendekezo la kufuta mkutano uliopangwa kufanyika saa nane mchana ili kuachiliwa kwa wanaharakati waliokamatwa. Pendekezo ambalo anadai kuwa limekataliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.