Pata taarifa kuu

Chad: Viongozi wawili wa waasi warejea kutoka uhamishoni kabla ya mazungumzo ya kitaifa

Hawa ni watu wawili wakuu wa makundi ya waasi tangu miaka kumi iliyopita ambao walirejea Ndjamena Alhamisi hii kushiriki katika ufunguzi wa mazungumzo jumuishi ya kitaifa unaofunguliwa Jumamosi hii. Timan Erdimi (67) na Mahamat Nouri (75), viongozi wawili wa waasi wenye asili sawa ya kisiasa.

Mahamat Nouri, kiongozi wa Muungano wa makundi ya waasi aliporejea Ndjamena baada ya miaka 16 akiwa uhamishoni, Agosti 18, 2022.
Mahamat Nouri, kiongozi wa Muungano wa makundi ya waasi aliporejea Ndjamena baada ya miaka 16 akiwa uhamishoni, Agosti 18, 2022. AFP - AURELIE BAZZARA-KIBANGULA
Matangazo ya kibiashara

Watu hawa wawili wana ukaribu na marais wawili wa zamani, anakumbuha mwandishi wetu wa Ndjamena, Madjiasra Nako. Mahamat Nouri alikuwa mmoja wa washirika wa karibu wa kwanza wa Hissène Habré katika miaka ya 1970 alipopigana na utawala wa François Tombalbaye. Wakati wa utawala wa Hissène Habré kutoka 1982 hadi 1990, alikuwa mmoja wa washirika wake wakuu.

Timan Erdimi, yeye, aliandamana na Idriss Deby mara tu alipoingia madarakani mwaka 1990 na kumsaidia kuanzisha mfumo wa kisiasa ambao ulitawala Chad kwa zaidi ya miaka thelathini.

Katikati ya miaka ya 2000, watu hao wawili, ambao walikuwa watu muhimu katika utawala wa Idriss Deby, waliasi muhula wa tatu ambao rais alikuwa akijiandalia kugombea na kuunda makundi mawili ya waasi kutoka Sudan. Kisha waliunda muungano na kufika kwenye lango la ikulu ya rais lakini walirudishwa nyuma kwa mashambulizi makali.

Baada ya kushindwa kijeshi mnamo mwezi  wa Mei 2009, walikimbilia uhamishoni: Mahamat Nouri nchini Ufaransa, na Timan Erdimi nchini Qatar.

Tangu mwezi wa Februari 2008, hii ni mara ya kwanza kwa watu hao wawili kuingia tena Ndjamena, safari hii bila silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.