Pata taarifa kuu

Jeshi la Tunisia latangaza kuwaua wanajihadi watatu

Jeshi la Tunisia limetangaza siku ya Ijumaa kuwa limewaua wanajihadi watatu kutoka kundi lenye mafungamano na kundi la Islamic State (IS) wakati wa operesheni katikati-magharibi mwa nchi hiyo.

Mamlaka inadai kuwa imepata mafanikio makubwa katika vita dhidi ya wanajihadi katika miaka ya hivi karibuni. Shambulio kubwa la mwisho lililotekelezwa na wanajihadi dhidi ya vikosi vya usalama ni la mwaka wa 2016 huko Ben Guerdane (kusini-mashariki) ambapo maafisa 13 wa vikosi vya usalama na raia 7 waliuawa, ikiwa ni pamoja na wanajihadi 55.
Mamlaka inadai kuwa imepata mafanikio makubwa katika vita dhidi ya wanajihadi katika miaka ya hivi karibuni. Shambulio kubwa la mwisho lililotekelezwa na wanajihadi dhidi ya vikosi vya usalama ni la mwaka wa 2016 huko Ben Guerdane (kusini-mashariki) ambapo maafisa 13 wa vikosi vya usalama na raia 7 waliuawa, ikiwa ni pamoja na wanajihadi 55. © REUTERS - ZOUBEIR SOUISSI
Matangazo ya kibiashara

Wanajihadi hao watatu, wanachama wa kundi la "Askari wa Ukhalifa", waliuawa asubuhi wakati wa operesheni ya jeshi katika eneo la Mont Salloum, karibu na Kasserine, mji ulio karibu na mpaka na Algeria, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Wizara ya Ulinzi.

Mnamo Agosti 12, wanajeshi wawili wa Tunisia walijeruhiwa kidogo katika majibizano ya risasi na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi katika eneo hilo, mamlaka imesema. Baada ya mapinduzi ya mwaka 2011 nchini Tunisia, nchi hiyo ilikumbwa na ongezeko la makundi ya wanajihadi ambayo yalifanya mashambulizi kadhaa ambayo yaliwauwa makumi ya watalii na vikosi vya usalama.

Mamlaka inadai kuwa imepata mafanikio makubwa katika vita dhidi ya wanajihadi katika miaka ya hivi karibuni. Shambulio kubwa la mwisho lililotekelezwa na wanajihadi dhidi ya vikosi vya usalama ni la mwaka wa 2016 huko Ben Guerdane (kusini-mashariki) ambapo maafisa 13 wa vikosi vya usalama na raia 7 waliuawa, ikiwa ni pamoja na wanajihadi 55.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.