Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

Kura ya maoni ya katiba Tunisia: Chombo cha uchaguzi chakumbwa na ukosoaji mkubwa

Baada ya kura ya maoni ya katiba ya Julai 25, iliyopelekea upande wa ndiyo kupata ushindi wa asilimia 94 ya kura zilizoiunga mkono Katiba mpya ya Rais Kaïs Saïed kwa kiwango cha ushiriki cha asilimia 30.5, wadau katika kampeni ya kura ya maoni walikuwa na miezi kadhaa kuwasilisha rufaa kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya mwisho. 

Maafisa wa uchaguzi wa Tunisia wakihesabu kura baada ya kura ya maoni kuhusu Katiba mpya hukoTunis, Julai 26, 2022.
Maafisa wa uchaguzi wa Tunisia wakihesabu kura baada ya kura ya maoni kuhusu Katiba mpya hukoTunis, Julai 26, 2022. AFP - FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa rufaa tatu zilizowasilishwa na vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia, mbili tayari zimekataliwa na Tume Huru ya Uchaguzi (ISIE) imekosolewa vikali.

Tangu ushindi wa “ndiyo” kwa rasimu ya Katiba ya rais wa Jamhuri, chombo cha uchaguzi kinachosimamia uandaaji wa kura ya maoni kimekuwa kikikabiliwa na shutuma nyingi za udanganyifu zinazofanywa na vyama vya upinzani.

Kisheria, ni mashirika au vyama vya kisiasa vilivyojiandikisha kufanya kampeni kuunga mkono kura ya "ndiyo" au ya"hapana" vinaweza kukata rufaa. Rufaa mbili kati ya hizi zilikataliwa wiki hii na mahakama ya utawala, rufaa ya tatu, ile ya chama cha Afek Tounes ambacho kilikuwa kimefanya kampeni ya kura ya "hapana" itachunguzwa Jumatatu wiki ijayo. Lakini kwa upande wa ISIE, ni suala la kuheshimisha majukumu iliyopewa.

Tangu kutangazwa kwa kura ya maoni, chombo hiki kimekuwa kikikabiliwa na utata na mashambulizi ya maneno, hususan na vyama vinavyopinga uhalali wa mchakato wa kura ya maoni katika kipindi cha kipekee. Wengi pia walikuwa wameitisha kususia kwa uchaguzi huo na kuitaka ISIE kusitisha maandalizi ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.