Pata taarifa kuu
TUNISIA- SIASA

Raia wa Tunisia wamepigia kura rasimu ya katiba mpya

Raia wa Tunisia, wamekuwa wakipigia kura rasimu ya katiba mpya, iliyopendekezwa na rais Kais Saied, mwaka mmoja baada ya kuivunja serikali na kusitisha shughuli za bunge, katika kile kilichoelezwa ni mpango wa kujilimbikizia madaraka.

Rais wa Tunisia Kais Saied
Rais wa Tunisia Kais Saied © AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema saa chache baada ya zoezi la kupiga kuanza, idadi ya watu waliojitokeza, walikuwa wachache, huku wapinzani wa rais Saied, wakiwaambia wananchi wasishiriki katika mchakato wanaosema utarejesha uongozi wa kidikteta katika nchi yao.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, kulikuwa na maandamano jijini Tunis, kupinga kufanyika kwa kura hii ya maoni, huku polisi wakiwakamata baadhi ya waandamanaji.

Kura hii ya maoni inafanyika mwaka mmoja kamili, baada ya rais Saied kuivunja serikali  na licha ya wapiga kura kutoonekana kujitokewa kwa wingi, rasimu hiyo ya Katiba inatarajiwa kupitishwa.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kufahamika siku ya Jumanne au Jumatano, katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, inayokabiliwa na kupanda kwa gharama ya masiha na ukosefu wa ajira hasa kwa vijana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.