Tunisia imepitisha katiba mpya, inayompa rais madaraka makubwa
Tunisia imepitisha katiba mpya, inayompa madaraka makubwa rais, baada ya kufanyika kwa kura ya maoni siku ya Jumatatu, ambayo idadi ndogo ya wapiga kura walijitokeza.
Imechapishwa:
Licha ya idadi ndogo ya wapiga kura ambayo ni asilimia 30, kujitokeza kushiriki kwenye zoewi hilo, waliunga mkono mabadiliko ya katiba kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi.
Wapinzani nchini humo waliosusia, zoezi hilo wamepinga ushindi huo na kusema matokeo yaliyotangazwa ni ya uongo na kilichotokea, kinarudisha nyuma hatua za demokrasia zilizopigwa.
Hata hivyo, rais Kais Saied, ameongoza wafuasi wake kusherehekea mabadiliko hayo anayosema ni ushindi wa nchi ya Tunisia, na inafungua ukurasa mpya wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika Kaskazini.
Katiba iliyopitishwa inatoa fursa kwa rais kuwa na madaraka makubwa, kinyume na katiba iliyopita, ambayo madaraka hayo yaligawanywa na bunge.
Mwaka mmoja uliopita, rais Saied, alivunja serikali na kusitisha vikao vya bunge katika kile kilichoonekana kama mapinduzi ya demokrasia nchini Tunisia.