Pata taarifa kuu
AFRIKA- UCHUMI.

Serikali za Afrika zinadaiwa karibu mara tatu na wakopeshaji binafsi

Ripoti mpya iliyochapishwa juma hili na shirika moja la utafiti kuhusu madeni nchini Uingereza, imesema kuwa, serikali za Afrika zinadaiwa karibu mara tatu na wakopeshaji binafsi kwenye nchi za Ulaya na China.

Shirika la fedha duniani IMF
Shirika la fedha duniani IMF AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Kwa kutumia takwimu za shirika la fedha duniani na benki ya dunia, taasisi hiyo inakadiria kuwa asilimia 35 ya madeni ya nje ya bara la Afrika yanadaiwa na benki, wathaminishaji mali na wafanyabiashara wamafuta, huku China pekee ikidai karibu asilimia 12 ya madeni hayo.

Kati ya dola za Marekani bilioni 444 zitakazolipwa na nchi za Kiafrika kati ya mwaka 2022 na 2028, dola bilioni 156 zitalipwa kwa wakopeshaji binafsi, China ikitarajiwa kulipwa bilioni 83.

Tangu kuzindiliwa kwa mpango wa nchi za G20 mwaka 2020, nchi tatu Ethiopia, Zambia na Chad, ziliomba kusaidiwa kifedha wakati huu madeni yake yakielekea kutovumilika kwa nchi hizi, huku hakuna hata moja iliyopokea msaada.

IMF imeonya nchi hizi kuchukua hatua za ubanaji matumizi au vinginevyo zitakumbwa na mdororo wakiuchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.