Pata taarifa kuu
NIGERIA- USALAMA

Nigeria: Wanajihadi wamewaua walinda usalama wanne

Maofisa wa polisi wanne akiwemo polisi mmoja wa akiba wameuawa katika shambulio la wanajihadi katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Gari la kundi la kigaidi la ISWAP Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Gari la kundi la kigaidi la ISWAP Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. AUDU MARTE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya wapiganaji hao wa Islamic State West Africa Province (ISWAP) inasema kuwa walishambulia kwa roketi msafara wa afisa wa serikali nchini humo Asheikh Mamman Gadai,wakati akiwa njia kurejea nyumbani kwake.

Kiongozi wa wapiganaji hao nchini humo Umar Ari ameeleza kuwa afisa huyo wa serikali hakujeruhiwa katika shambulio hilo.

Shambulio hilo limetokea katika kijiji cha Mile 40 katika barabara kuu ya Maiduguri- Monguno.

ISWAP imekuwa ikitekeleza mashambulio kwa misafara ya maofisa wa usalama pamoja na kuwapora na kuwaua raia kwenye barabara hiyo ya Maiduguri- Monguno.

Kutokana na kuongezeka kwa mashambulio ya wanajihadi katika barabara hiyo poliisi wamelazimika kuimarisha usalama kama njia moja ya kuwalinda raia japokuwa mashambulio yameendelea kuongezeka.

Zaidi ya watu 40,000 wameuawa wengine zaidi ya milioni 2.2 wakiyakimbia makwao kwa kuhofia kushambuliwa kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Nchi jirani na Nigeria zikiwemo, Niger, Chad na Cameroon nazo pia zikiripotiwa kuathiriwa na shughuli zainazoendelezwa na makundi ya wapiganaji nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.