Pata taarifa kuu

Chad: Umoja wa Afrika katika ziara ya kidiplomasia kabla ya mazungumzo ya kitaifa

Chad inajiandaa kuwa pokea viongozi kadhaa wa Umoja wa Afrika wiki hii kuanzia Jumatatu hii, Agosti 15. Siku tano kabla ya kufunguliwa kwa mazungumzo shirikishi, ambayo yatawezesha kurejea kwa utaratibu wa kikatiba, rais wa sasa wa Umoja wa Afrika, Macky Sall ambaye pia ni wa Senegal, na maafisa wakuu wa shirika la kikanda watakuwa Ndjamena kwa misheni ya kidiplomasia.

Rais wa Senegal Macky Sall anatarajiwa kzuru mjini Ndjamena, Chad, Agosti 15, 2022,  kama mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika.
Rais wa Senegal Macky Sall anatarajiwa kzuru mjini Ndjamena, Chad, Agosti 15, 2022, kama mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika. AP - JOHN ANGELILLO
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, Balozi Bankole Adeoye, ambaye aliwasili Chad mjini Ndjamena Jumapili Agosti 14, amesema ziara ya wajumbe hao itakuwa ni tukio la ujumbe wa kutathmini hali nchini Chad. Kwa lengo hili, atakutana na wahusika wote wa kisiasa, upinzani na wengi bungeni, pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kiraia.

Siku moja baada ya kifo cha Rais wa Chad Idriss Déby, Aprili 2021, Umoja wa Afrika ulimeamua kutoichukulia vikwazo serikali ya kijeshi iliyowekwa madarakani huko Ndjamena bali kuiunga mkono, mradi tu "mazungumzo yasiyo na masharti yafunguliwe kati ya serikali ya mpito na wadau wote wanaohusika, vikiwemo vyama vya siasa vya upinzani na makundi yenye silaha”.

Umoja wa Afrika pia ulitaka mamlaka iliopo kuheshimu miezi 18 ya kipindi cha mpito, na pia ulifahamisha kwamba viongozi wa kipindi hiki cha mpito hawapaswi kuwa wagombea katika uchaguzi ujao.

Hata kama ni ziara rasmi ya nchi mbili, rais wa Senegal Macky Sall atalazimika kujadiliana na mamlaka ya Chad kuhusu mahitaji ya Umoja wa Afrika kabla ya kuwasili kwa Moussa Faki Mahamat, rais wa tume ya taasisi hiyo. Atakuwa na jukumu la kuuwakilisha Umoja wa Afrika katika ufunguzi wa mdahalo wa kitaifa utakaofanyika Jumamosi Agosti 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.