Pata taarifa kuu

Tiémoko Meyliet Koné, makamu wa rais mpya wa Côte d'Ivoire

Côte d'Ivoire ina makamu wa rais mpya: mwanabenki mkuu Tiémoko Meyliet Koné ameteuliwa Jumanne na mkuu wa nchi Alassane Ouattara kwenye wadhifa huu ambao umekuwa wazi kwa karibu miaka miwili, huku waziri mkuu Patrick Achi akiteuliwa tena.

Makamu wa rais mpya wa Côte d'Ivoire, Tiémoko Meyliet Koné.
Makamu wa rais mpya wa Côte d'Ivoire, Tiémoko Meyliet Koné. AFP - ERIC PIERMONT
Matangazo ya kibiashara

Gavana wa Benki Kuu ya Mataifa ya Afrika Magharibi (BCEAO) tangu 2011, Bw. Koné ni "mchumi mahiri" na "mtaalamu bora wa teknolojia", kulingana na Alassane Ouattara ambaye ametangaza uteuzi wake kwa wabunge waliokusanyika kwa mabunge yote mawili (Baraza la Congress na Bunge la Seneti) katika mji mkuu wa kisiasa Yamoussoukro.

"Tiémoko Meyliet Koné ni mtu wa makubaliano na mwenye busara ambaye ninamuamini kikamilifu," ameongeza Alassane Ouattara. Akiwa ameidhinishwa na wabunge, Bw. Koné alipanda jukwaani ili kupeana mikono na rais. Atakula kiapo siku chache zijazo.

Alizaliwa mwaka wa 1949, mwanauchumi huyu ambaye hajulikani sana na umma kwa ujumla ataondoka Benki ya BCEAO, ambayo alikuwa gavana wake tangu mwaka 2011 na ambapo alisimamia mageuzi yanayoendelea ya faranga ya CFA. Kabla ya kuwa gavana wa BCEAO, alikuwa na kazi ndefu ndani ya taasisi hiyo.

Pia alikuwa na taaluma fupi ya kisiasa nchini Côte d'Ivoire: alikuwa mkurugenzi kwenye ofisi ya Waziri Mkuu Guillaume Soro kati ya mwaka 2007 na 2010, Waziri wa Ujenzi, kisha mshauri maalum wa Rais wa Jamhuri Alassane Ouattara, anayesimamia uchumi na fedha.

"Huyu ni mtu ambaye ameonyesha sifa zake za kibinafsi na kitaaluma katika nyadhifa zote za juu alizoshikilia katika utawala wa umma, katika serikali ya Côte d'Ivoire na nje ya Côte d'Ivoire", ameongeza mkuu wa nchi.

Nafasi ya makamu wa rais, mahali muhimu katika mageuzi ya mwisho ya katiba ya mwaka 2016, ilikuwa wazi tangu Julai 2020 baada ya kujiuzulu kwa Daniel Kablan Duncan kwa "sababu za kibinafsi".

Uteuzi wa makamu wa rais ulitarajiwa kwa siku chache, baada ya kujiuzulu kwa serikali Jumatano iliyopita ambayo iliashiria mabadiliko ya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.