Côte d’Ivoire: Raia watiwa wasiwasi kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa
Nchini Côte d'Ivoire, kupanda kwa bei za bidhaa za kimsingi kumesababisha raia kutoa maoni mbalimbali. Mafuta ya kupikia, nyama, mchele, petroli, au vitoweo vimepanda bei hivi majuzi kuanzia %10 hadi 40, huku mwaka wa 2021 tayari ukiwa na ongezeko la jumla la bei.
Imechapishwa:
Shirikisho la wanunuzi nchini Côte d'Ivoire sasa linaiomba serikali kuchukua hatua kutokana na kuzorota kwa ununuzi.
Suala hili limekuwa ni gumzo nchini Côte d'Ivoire. Ongezeko la hivi majuzi la bei ya mafuta, kutoka faranga za CFA 615 hadi faranga 635, na bidhaa za kimsingi, hususan nyama ya ng'ombe na mafuta ya kupikia, vinauzwa kwa bei ghali . Jean-Philippe Koffi, kiongozi wa muungano wa mashirika ya wanunuzi nchini Côte d'Ivoire, sasa anaiomba serikali kuchukua hatua. Kulingana na yeye, kuzuiwa kwa muda wa bei ya baadhi ya bidhaa za watumiaji haitoshi tena.