Pata taarifa kuu

Washington yaidhinisha mauzo ya dola bilioni 1 ya vifaa vya kijeshi kwa Nigeria

Washington imeidhinisha uuzaji wa helikopta za mashambulizi na vifaa vya kijeshi kwa Nigeria kwa thamani ya karibu dola bilioni 1. Kwa hivyo Washington inathibitisha uungaji wake mkono wa kijeshi kwa mshirika wake wa kimkakati katika Afrika Magharibi, ambayo imekuwa ikikabiliwa kwa miaka mingi na uasi wa jihadi Kaskazini mwa nchi.

Picha iliyotolewa na kikosi cha majini cha Marekani, U.S. Marine, Aprili 17, 2017 inaonyesha ndege aina ya AH-1Z Viper ikijiandaa kutua katika eneo la Chocolate Mountain, California. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Alhamisi (Aprili 15) iliidhinisha mauzo makubwa ya helikopta za mashambulizi kwa Nigeria kwa karibu dola bilioni 1.
Picha iliyotolewa na kikosi cha majini cha Marekani, U.S. Marine, Aprili 17, 2017 inaonyesha ndege aina ya AH-1Z Viper ikijiandaa kutua katika eneo la Chocolate Mountain, California. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Alhamisi (Aprili 15) iliidhinisha mauzo makubwa ya helikopta za mashambulizi kwa Nigeria kwa karibu dola bilioni 1. AP - Cpl. Harley Robinson
Matangazo ya kibiashara

Bunge la Marekani lilichelewesha uuzaji huo kutokana na wasiwasi juu ya ahadi za Abuja za kulinda raia katika maeneo ambayo makundi yenye silaha yanaendesha shughuli zake.

Helikopta kumi na mbili za AH-1Z Viper, lakini pia mifumo ya mwongozo na vifaa vya vinavyosaidia kuona usiku, silaha pamoja na kifurushi cha mafunzo kwa marubani wa Nigeria, hivi ndivyo Washington itatoa kwa Abuja.

Hii, kulingana na mamlaka ya Marekani, ni "kuiwezesha Nigeria vyema zaidi ili kuendeleza utulivu wa kikanda na kuimarisha ushirikiano na Marekani na washirika wengine wa Magharibi". Ni wazi kwamba Washington inaunga mkono mapambano yanayoongozwa na Nigeria dhidi ya makundi ya wanajihadi wenye silaha.

Mkataba huu muhimu ulikuwa umecheleweshwa na Bunge la Marekani, likiwa na shauku ya kupata ahadi kutoka kwa viongozi wa Nigeria kulinda vyema raia katika maeneo yenye matatizo.

Mwaka jana, Abuja pia ilipokea ndege ya kwanza ya mashambulizi ya ardhini aina ya Super Tucano, mkataba ambao awali ulizuiwa na Barack Obama, kufuatia mashamùbulizi y anga ya Nigeria kwenye kambi ya wakimbizi, na kisha kuzuiwa na mrithi wake, Donald Trump.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.