Pata taarifa kuu

Nigeria: Rais Buhari aomba radhi kwa kukatika kwa umeme nchini

Nigeria inakabiliwa na tatizo kubwa la nishati. Nchi hii haina umeme tangu Jumatatu, Machi 14, 2022. Mamlaka inakiri kuwepo kwa kiwango kidogo cha uzalishaji.Zaidi ya 80% ya kampuni na mashirika makubwa nchini Nigeria yanaendeshwa na gesi asilia. Rasilimali ambayo bei imeongezeka kwa kasi tangu mgogoro nchini Ukraine. Angalau vituo kadhaa vya umeme vimeshindwa kufanya kazi au vimezalisha kiwango kidogo cha umeme.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. © Nigeria presidency
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwaka wa 2014 na ubinafsishaji wa mfumo wa nishati wa Nigeria, nchi hiyo imekabiliwa na uhaba wa mara kwa mara wa gesi kwa ajili ya mitambo ya kuzalisha umeme kwa sababu ina faida zaidi kwa wazalishaji wa gesi kuuza nje ya nchi. Baadhi ya waangalizi pia wanataja vitendo vya uharibifu kwenye mitambo ya kuzalisha umeme ndani ya nchi.

Katika barua iliyochapishwa katika vyombo vya habari vya Nigeria, Rais Muhammadu Buhari anaomba radhi kwa raia wenzake na kuahidi kutatua mgogoro huo katika siku zijazo. Ikiwa 40% ya watu tayari hawana umeme, nchi nzima sasa inafanya kazi na jenereta zinazotumia mafuta.

Kutegemea bei katika masoko ya kimataifa

Hili litasababisha tatizo la pili kwani bei ya petroli pia imepanda kutokana na mzozo wa Ukraine. Hata hivyo, Nigeria inazalisha kiasi kikubwa cha mafuta, lakini kwa vile haina njia za kiufundi za kuyasafisha, kwa hiyo inalazimika kuagiza mafuta mengi kutoka nje na kuzingatia bei ya soko la dunia.

Mashahidi kadhaa, hasa wafanyabiashara waliohojiwa na RFI, wanasema kwamba ongezeko hili la bei ya mafuta linaonekana katika sekta zote za maisha ya kila siku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.