Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Nigeria: Ishirini na nne waangamia katika shambulio la watu wenye silaha Benue

Watu wenye silaha, wamewauwa watu 24 katika jimbo la Benue nchini Nigeria, wakati huu eneo hilo linapoendelea kushuhudia utovu wa usalama.

Rais Muhammadu Buhari ameelani kuendelea kwa mauji haya na kuahidi waliohusika wataadhibiwa vikali, wakati huu akiendelea kupata shinikizo za kukabiliana na hali ya utovu wa usalama nchini humo.
Rais Muhammadu Buhari ameelani kuendelea kwa mauji haya na kuahidi waliohusika wataadhibiwa vikali, wakati huu akiendelea kupata shinikizo za kukabiliana na hali ya utovu wa usalama nchini humo. AFP
Matangazo ya kibiashara

Gavana wa jimbo hilo, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, wakati huu machafuko yakiendelea kushuhudiwa kwa sababu ya kupigania ardhi na maji kati ya wafugaji na wakulima.

Hali hii imesababisha watu wenye silaha kuwavamia watu, kuwauwa, kuwateka na kuwabaka wanawake na wasichana.

Kuhusu mauaji haya,  wafugaji kutoka kabila la Fulani, walivamia na kuwauwa watu wanane katika kijiji cha Guma na wengine 16 katika eneo la Tiortyu.

Jumapili iliyopita watu wenye silaha waliwauwa watu wengine zaidi ya 100 katika jimbo la Plateau.

Rais Muhammadu Buhari ameelani kuendelea kwa mauji haya na kuahidi waliohusika wataadhibiwa vikali, wakati huu akiendelea kupata shinikizo za kukabiliana na hali ya utovu wa usalama nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.