Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Tukio la shambulizi dhidi ya treni Kaduna laendelea kuwa gumzo Nigeria

Kamishna wa polisi katika jimbo la Kaduna, Samwel Aruwan, amesema abiria waliojeruhiwa katika tukio hilo wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali mbali mbali, huku jeshi likiendelea na uokoaji. 

Shirikisho la reli la Nigeria limesema huduma za reli kutoka Abuja kuelekea Kaduna zimesitishwa kwa muda.
Shirikisho la reli la Nigeria limesema huduma za reli kutoka Abuja kuelekea Kaduna zimesitishwa kwa muda. © AP
Matangazo ya kibiashara

Tukio hili la Jumatatu usiku kwenye treni ambayo ilikuwa imebeba takriban abiria  970, limeonekana kuwa ni ongezeko lingine la magenge ya wahalifu yanayojulikana katika eneo hilo kama majambazi. 

Shirikisho la reli la Nigeria limesema huduma za reli kutoka Abuja kuelekea Kaduna zimesitishwa kwa muda. 

Siku mbili zilizopita, watu waliokuwa wamejihami walimvamia na kumuua mlinzi katika uwanja wa ndege wa Kaduna kabla ya vikosi vya jeshi kuingilia kati, ambapo pia mwezi Oktoba wahalifu walivamia njia hiyo ya reli wakitumia vilipuzi. 

Magenge ya majambazi yamekuwa yakiwahangaisha raia katika majimbo ya kaskazini magharibi na kati nchini humo, wakitekeleza mauaji, utekaji nyara, kuvamia vijiji na hata kuiba mifugo. 

Jeshi la Nigeria limekuwa llikitekeleza operesheni na hata uvamizi wa angani ili kuyaondoa magenge hayo kutoka kwa kambi zao msituni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.