Pata taarifa kuu
Africa - Baa la Njaa

Raia millioni 346 wanakabiliwa na njaa barani Africa.

Zaidi ya raia millioni 346 barani Africa wanakabiliwa na baa la njaa, baadhi ya familia zikilazimika kupata chakula mara moja kwa siku, hali ikitarajiwa kuwa mbaya zaidi iwapo hatua za dharura hazitachukulia, kamati ya kamataifa ya shirika la msalaba mwekundu, ICRC, imesema.

Raia wakipokea misaada kutoka kwa Kamati ya kimataifa ya Shirka la msalaba mwekundu
Raia wakipokea misaada kutoka kwa Kamati ya kimataifa ya Shirka la msalaba mwekundu REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Kwa mjibu wa mkurugenzi wa shughuli za kimataifa wa ICRC, Dominik Stillhart, família nyingi zinakabiliwa na njaa, huku watoto wakifariki kutokana na Utapilia mlo, hali hii ikiwa mbaya zaidi katika mataifa ya, Burkina Faso, Mauritania, Somalia, Ethiopia,Kenya, Sudan Kusini, DRC, Sudan, Nigeria, Jamhuri ya Africa ya Kati, Chad, Cameroon, Niger na Mali.

Stillahart amesema wanaimarisha shughuli za kutoa misaada katika mataifa yalioathirika ili kuokoa jamii ambazo zimeathirika na hali hii, na ukosefu wa maji.

00:23

DOMINIC STIILHART SNIP 05 04 2021 KUHUSU MHALI NJAAA

ICRC, inasema hali hii kanda ya Africa mashariki, imetokana na kipindi kirefu cha kiangazi, vita ambavyo vimesababisha raia kukimbia makwao na kuongezeka kwa bei ya vyakula na mafuta, wakati huu pia mataifa mengi yakikabiliwa na hali ngumu ya uchumi kutokana athari ya janga la Uviko 19.

Wafadhili zaidi.

ICRC, inatoa wito kwa wafadhili zaidi kujitokeza, ikiwemo serikali na mashirika ya kibinadamu ili kusadia kutafuta suluhu la kudumu kwa wakati huu.

Kwa mjibu wa Ann Kilimo ni mratibu wa mawasiliano wa ICRC, jijini Nairobi, ni kwamba hali huenda ikawa mbaya zaidi kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Ukraine na Urusi, kwani mataifa mengi yanategemea ngano kutoka Ukraine.

00:26

ANNE KILIMO SNIP 05 04 2022 KUHUSU NJAA AFRICA

Kwa sasa ICRC, inashirikiana na  mashirika mengine kutoa misaada kwa mataifa ambayo yameathirika zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.