Pata taarifa kuu

Somalia yahitaji msaada wa kutosha kukabiliana na baa la njaa

Somalia inaomba msaada wa kimataifa, ili kuwalisha watu Milioni 6 nukta 9 wanaokabiliwa na baa la njaa na uhaba wa maji. 

Somalia inakabiliwa na ukame unaoendelea.
Somalia inakabiliwa na ukame unaoendelea. © AP Photo/Elias Meseret
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble amesema uhaba wa chakula kumesababisha mamilioni ya raia wa Somalia kuyakimbia makwao kwenda kutafuta chakula na maji safi kwa ajili ya matumizi yao. 

Roble amesema msaada wa haraka wa kibinadamu unahitajika ili kuwasaidia watu wanaokabiliwa na changamoto hii, ambayo inaelezwa kuwa mbaya tangu nchi hiyo ilipokabiliwa na ukame mwaka 2011. 

Mpaka sasa watu watatu, wamepoteza maisha kwa  kukosa chakula, Kusini Magharibi mwa nchi hiyo êneo ambalo kwa sasa maelfu hawana chakula. 

Wito huu unakuja baada ya Umoja wa Mataifa kuonya kuwa mamilioni ya wat nchini Somalia wapo katika hatari ya kuthiriwa na baa la njaa. 

Kundi la Al Shabab limechukua hali hii, kudhibiti maeneo yenye uhaba wa chakula na maji na hivyo kutishia usalama wa nchi hiyo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.