Pata taarifa kuu
GUINEA-HAKI

Fofana na mawaziri watatu wa zamani wa Guinea wafungwa kwa "ubadhirifu"

Ibrahima Kassory Fofana, Waziri Mkuu wa Guinea hadi mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2021, pamoja na mawaziri watatu wa zamani wa rais aliyeondolewa madarakani Alpha Condé wameshtakiwa Jumatano kwa tuhuma za "ubadhirifu" wa mali ya umma na kufungwa huko Conakry,  mmoja wa mawakili wao ameliambia shirika la habari la AFP.

Ibrahima Kassory Fofana, mnamo Oktoba 2015 huko Conakry (picha ya zamani).
Ibrahima Kassory Fofana, mnamo Oktoba 2015 huko Conakry (picha ya zamani). © CELLOU BINANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Walishtakiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma na kupelekwa gerezani," amesema Wakili Salifou Béavogui, mkuu wa kundi la wanasheria. Mbali na Bw. Fofana, maafisa wa zamani waliofungwa ni Waziri wa zamani wa Ulinzi Mohamed Diané, yule wa Mazingira Oyé Guilavogui na yule wa hidrokaboni Zakaria Coulibaly. Mahakama itatoa uamuzi kuhusiana ma mashitaka dhidi yao Jumatatu, amesema.

"Tunafiriki kwamba hawakustahili kwenda jela kwa sababu hawajakutwa na hatia, wako katika dhana ya kutokuwa na hatia " , ameongeza Wakili Béavogui.

Maafisa hao wanne wa zamani wamefikishwa Jumatano wiki hiii mbele ya ofisi ya mashtaka ya Mahakama ya Makosa ya Kiuchumi na Kifedha (CRIEF), iliyoundwa upya na viongozi wa mapinduzi waliompindua rais Condé mnamo Septemba 5 baada ya zaidi ya miaka kumi madarakani.

Hapo awali walikuwa wamesikilizwa kwa siku tatu na wachunguzi. Makosa ambayo wanashtakiwa hayajabainishwa.

Ibrahima Kassory Fofana, mkuu wa serikali kuanzia Mei 2018 hadi mapinduzi ya Septemba 2021, alikuwa ameteuliwa Machi 31 kama kiongozi wa chama tawala cha zamani chini ya Bw. Condé, hadi mkutano ujao. Bw. Diane alikuwa mmoja wa maafisa wakuu chini ya Bw. Condé.

Wanajeshi waliochukuwa madaraka kwa nguvu wamefanya vita dhidi ya ufisadi ikizingatiwa kuwa moja ya vita vyao kuu vilivyotangazwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.