Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA

Majadiliano ya kitaifa yaanza Guinea

Kongamano la Kitaifa kujadili juu ya mfumo mpya wa taasisi za serikali nchini nchini Guinea linaanza Jumanne hii, chini ya uongozi wake Rais wa mpito, kanali Mamady Doumbouya

Mamady Doumbouya, rais wa mpito wa Guinea.
Mamady Doumbouya, rais wa mpito wa Guinea. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Kongamano hili linalenga kujenga mfumo mpya juu ya namna ya kuendeleza taasisi za serikali nchini humo kama ilivyokubaliwa na asasi za kiraia, pamoja na wawakilishi wa vyama vya kisiasa vinavyounga mkono serikali ya mpito na upinzani.  

Baada ya kuingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi, Kanali Mamady Doumbouya mwezi Oktoba mwaka uliopita,  aliahidi kuongoza mashauriano ambayo alisema ni ya kuombana msamaha na kuambiana Ukweli, ili kuijenga demokrasia ya taifa hilo, kama alivyosema mwishoni mwa mwaka jana.

Mapendekezo yatakayotolewa kupitia kongamano hili yatajumuishwa kwa pamoja na yale yaliyochapishwa mwaka 2016 ambayo yanasisitizia umuhimu wa kuitetea Katiba na kuhakikisha utawala wa kiraia unarejeshwa nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.