Pata taarifa kuu
GUINEA-MAZUNGUMZO

Guinea: Utawala wa kijeshi wateua kamati inayoongozwa na imam na askofu mkuu

Nchini Guinea, mamlaka inayotawala imeunda Kamati ya Kitaifa (CNA) ambayo itaongozwa na imamu na askofu mkuu kwa ajili ya kufanya mkutano wa upatanisho uliozinduliwa Machi 22 kwa wiki sita

Kanali Mamadi Doumbouya, kiongozi wa utawala wa kijeshi, Conakry Septemba 10, 2021.
Kanali Mamadi Doumbouya, kiongozi wa utawala wa kijeshi, Conakry Septemba 10, 2021. REUTERS - SALIOU SAMB
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa utawala wa kijeshi, Kanali Mamady Doumbouya aliteua, Ijumaa, watu 31 kuunda CNA, wakiwemo makasisi, wanasheria, wanahabari, wanahistoria, wanasosholojia, au watu kutoka ulimwengu wa utamaduni, imetangaza televisheni ya taifa RTG.

Imamu Mkuu Elhadj Mamadou Saliou Camara wa Msikiti wa Fayçal huko Conakry na Askofu Mkuu wa Conakry, Vincent Koulibaly, watakuwa watasimamia Kamati ya kitaifa (CNA) kuongoza mchakato wa kuandaa mkutano huo, kulingana na chanzo hicho.

Vikao hivyo, vilivyofunguliwa Jumanne, vimewasilishwa na utawala wa kijkeshi kama fursa ya "kihistoria" ya kuponya majeraha ya siku za nyuma zenye matatizo, lakini mashirika mengi ya kisiasa yameamua kuvisusia.

Hata hivyo, Kanali Doumbouya bado hajasema lolote kuhusu tarehe ya mwisho ambayo anakusudia kuheshimu ahadi yake ya kurudisha mamlaka kwa raia waliochaguliwa.

Siku ya Ijumaa, ECOWAS ilitoa uamuzi kwa Guinea, ikitishia kuiwekea vikwazo zaidi ikiwa haitawasilisha "ratiba ya mpito inayokubalika" kabla ya Aprili 25, 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.