Pata taarifa kuu

Kumi na nane wafariki baada ya kuangukiwa na udongo katika eneo la Gaoual

Watu 18 wamepoteza maisha Magharibi mwa nchi ya Guinea baada ya kuporomoka kwa mgodi wa dhahabu usiokuwa rasmi. 

Moja ya migodi nchini Guinea.
Moja ya migodi nchini Guinea. © Business Wire 2018
Matangazo ya kibiashara

Afisa wa serikali Ousmane Gaoual Diallo amesema tukio hilo lilitokea, siku ya Jumatatu katika eneo la Gaoual, Kilomita 386 kutoka jiji kuu Conakry. 

Inahofiwa kuwa huenda miili zaidia ikapatikana, baada ya hiyo 18 wakati huu operesheni ikiendelea. 

Mkasa huu umetokea katika êneo hilo ambalo katika miezi ya hivi karibuni, wachimbaji wamekuwa wakitafuta dhahabu na ajali kama hizi zimekuwa zikitokea mara kwa mara. 

Mwezi Mei mwaka uliopita, watu wengine 15  walipoteza maisha baada ya kuporomoka kwa mgodi mwingine wa dhahabu katika êneo la Siguiri Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.