Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU-USALAMA

Guinea-Bissau: Milio ya risasi yasikika katika mji mkuu, redio ya kibinafsi yalengwa

Wiki moja baada ya shambulio kwenye makao makuu ya serikali, milio ya risasi imesikika leo Jumatatu asubuhi huko Bissau. Inaonekana kwamba kituo cha redio cha kibinafsi kimelengwa.

Redio ya kibinafsi Capital FM, mojawapo zinazokosoleawa na mamlaka ya asa nchini Guinea-Bissau, imelengwa.
Redio ya kibinafsi Capital FM, mojawapo zinazokosoleawa na mamlaka ya asa nchini Guinea-Bissau, imelengwa. © Mussá Baldé
Matangazo ya kibiashara

Redio Capital FM inayopatikana katika eneo la Bairro Militar, kituo cha redio kinachochukuliwa kuwa karibu na upinzani wa PAIGC ndicho ambacho kimelengwa. Kulingana na mashahidi waliohojiwa na RFI, magari mawili ya watu waliovalia sare za kijeshi yalifika karibu na kituo cha redio asubuhi na kuanza kufyatua risasi.

Watatu wajeruhiwa

Watu watatu wamejeruhiwa na vifaa viliharibiwa lakini idadi bado haijathibitishwa, kulingana na Moustafa Keita, Mkurugenzi wa redio. Wafanyakazi kwenye redio hiyo wameelezea kutoelewa kwao kufuatia shambulio hili, na hii sio mara ya kwanza kwa ka ituo chCapital FM kulengwa.

Polisi wamewasili katika eneo la tukio na jengo hilo haliingiliki, huku wakazi wa kitongoji hicho wakiwa wamekusanyika mbele ya redio.

Biashara ya dawa za kulevya

Tukio hili linatokea chini ya wiki moja baada ya shambulio dhidi ya makao makuu ya serikali. Kufuatia jaribio la mapinduzi lililolaaniwa na rais, mamlaka ilishutumu kitendo kilichofanywa na watu wanaohusishwa na biashara ya madawa ya kulevya na mamluki, wakundi la "waasi wa Casamance", kulingana na msemaji wa serikali.

Matukio haya mapya yanakuja baada ya siku za hivi karibuni kushuhudiwa utulivu huko Bissau.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.