Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU-USALAMA

Hali ya utulivu yarejea Guinea-Bissau baada ya jaribio la mapinduzi, ECOWAS yatuma wanajeshi

Siku chache baada ya jaribio la mapinduzi ambalo bado ishara zake zinaonekana katika ikulu ya rais huko Bissau, ECOWAS iliamua katika mkutano wake wa siku ya Alhamisi kutuma wanajeshi nchini humo.

Mwanajeshi karibu na makao makuu ya serikali huko Bissau, Februari 1, 2022.
Mwanajeshi karibu na makao makuu ya serikali huko Bissau, Februari 1, 2022. AFP - AFPTV TEAMS
Matangazo ya kibiashara

Wakuu wa nchi za ECOWAS walitangaza kuwa wanajeshi watatumwa Guinea-Bissau bila kutaja ratiba au idadi ya wanajeshi watakaotumwa. Tangazo hilo linafuatia machafuko ya Jumanne, shambulio dhidi ya makao makuu ya serikali lililoelezewa kama "jaribio la mapinduzi", ambapo watu 11 waliuawa, kulingana na ripoti rasmi.

Rais Umaro Sissoco Embalo amewapokea Ijumaa hii asubuhi wawakilishi wa vyama vya siasa waliofika kueleza "mshikamano" wao.

Rais alijificha kwenye chumba cha kiufundi

Kulingana na maafisa wa kijeshi, Rais Umaro Sissoco Embalo alitoka katika chumba hiki wakati wa shambulio kupitia mlango wa nyuma ili kujificha kwenye chumba cha kiufundi, nyuma ya mitambo ya umeme. Na katika chumba hiki, kwenye dirisha, unaweza kuona kasha za risasi. Kwa upande mwingine, ofisi ya mkurugenzi wa fedha iliporwa kabisa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.